Naomba Nijuzwe kama ni kweli kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi

Tatizo liko wapi boss? Kama sisi tumeshindwa kuweka mipango miji ya kueleweka kosa ni la kwetu, huwezi kulazimisha mtu akae uswazi ambapo jengo likishika moto hata zimamoto lishindwe kufika huko. Haiwezekani mtu alazimishwe kukaa sehemu ya hovyo kisa uzalendo.

Kiufupi hii Dar inatakiwa ipangwe upya ipangike, jiji limekaa kiwakiwaki sana.

Hapo suluhisho ni kuvunja uswazi zote jijini, unapandisha apartments wale waliovunjiwa unawapa kipaumbele cha kwanza kupewa vyumba.
Tukishindwa hilo basi tuipime ardhi ya nchi nzima kuzuia kilicho tokea huku Dar kusambaa nchi nzima miaka ijayo.
Tushachelewa huko mikoani ujenzi holela unaendelea kwa kasi ya kutisha.
 
Kuna wengine wapo Masaki wamechukua nyumba aliyokuwa anakaa Ruge na kuanzisha chimbo la bata linaitwa bbq and chill..

Inawezekana ni kweli wapowapo..
 
Tushachelewa huko mikoani ujenzi holela unaendelea kwa kasi ya kutisha.
Hatujachelewa kihivyo, nchi ndio kwanza ina watu milioni 60 ukilinganisha na Nigeria milioni 200 huko. Tukianza sasa au ndani ya miaka mitano, itakuwa safi.

Changamoto inayokuja na kufanya utekelezaji uwe mgumu ni kwamba hii kitu haipo kwenye interest za wanasiasa. Maana ukiingiza pesa kwenye upimaji halafu mwananchi anataka barabara, akirudi kwa mpiga kura aseme amesaidia kupima ardhi ya nchi, kwa mwananchi ataona michosho. Lakini madhara yake yatakuwa makubwa na gharama yake itakuwa kubwa zaidi kurekebisha nchi kwa wakati huo na itakuwa too late kwa vizazi vijavyo ambao nao wataishia kutulaumu sisi na kutuona tulikuwa mazumbu kuku.

Pia likifanikiwa suala hili ya kuipima nchi nzima, itasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya kodi ya majengo kirahisi zaidi. Maana mitaa yote itakuwa ya kueleweka. Kuliko hii ya sasa mpka mjumbe anachanganyikiwa kujua nyumba za mtaa wake mwenyewe.

Embu fikiria maeneo aliyotuachia mzungu kama Obay na Masaki, kiukweli tumeshindwa kuendeleza maeneo yenye hadhi ya hivyo labda kidogo Mbweni, Bunju beach na maeneo mengine machache sana.
 
Waje tu ila serikali ijipange zaidi kuwavuna utaalam na ujuzi walionao kusaidia kupunguza ujinga uliopo nchini. Yale maeneo ambayo serekali imeshindwa kupeleka waalimu waende wakajitolee kufundisha, michezo, sanaa n.k. Wasiishie tu mijini 'kula bata'


Kuna huyu anaishi arusha,ameanza kufundisha arts,ni muda mzuri sana wa kuwatumia hawa,serikali isiwaache hivi hivi
 
Hatujachelewa kihivyo, nchi ndio kwanza ina watu milioni 60 ukilinganisha na Nigeria milioni 200 huko. Tukianza sasa au ndani ya miaka mitano, itakuwa safi...
Serekali yetu inashindwa kabisa kujipambanua, wanasiasa wametegesha matumbo yao kuvizia pesa za wizi, misaada na rushwa. Sijui ni laana ama ni nini
 
Nenda Youtube, tafuta jamaa anaitwa "GoBlackToAfrica".

Utaona jamaa anaifagilia sana Bongo.

Na wenzake wanamfuatilia sana.

Yani wizara zetu za Utalii wanazembea sana, mtu kama huyu walitakiwa wamtumie kufanya promotion ya utalii kwa Wamarekani, hususan weusi, waje wapaone Tanzania na wakitaka kuhamia wahamie.
 
watu hawaamini ila ndio ukweli unashangaza sana.

juzi naongea na jamaa mmoja anafanya kazi ubarozi,anakwambia hakuna kitu kigumu kama afisa wa ubarozi humo kuambiwa anatakiwa aondoke nyumbani muda umekwisha,huwa wanalia sana...
Sasa bongo maisha ni rahisi kwao cause wanalipwa mpunga mrefu alafu gharama za kuishi zipo chini. Halafu bongo hamna mchakamchaka kama wa maisha kama mtoni. So kufanya kazi ubalozini ni kama Vacation kwao
 
Kuna mmoja wiki ijayo anatia timu,kaniambia hamjui yeyote bonge,anakuja kuwekeza Tz,niwe mwenyeji wake ,nisiwe mpigaji tu ,andazi la 200,,nimwambie 2000
 
Sasa bongo maisha ni rahisi kwao cause wanalipwa mpunga mrefu alafu gharama za kuishi zipo chini.
Alafu bongo hamna mchakamchaka kama wa maisha kama mtoni. So kufanya kazi ubalozini ni kama Vacation kwao
mtu kunyong'onyea inaweza kuwa kawaida,ila anapolia kabisa ndipo maajabu yalipo.
 
Huyu kaacha Deni la zaidi ya laki 7 home maana tuna Hostel za wageni.

Wabongo sio kila anaetoka ng'ambo ana hela wengine Ni njaa. Nina experience Sana na Hawa watu maana home tuna Hostel za wageni ...

Nawaomba muwafuate wamiliki wa hostels za wageniuwaulizie tabia za Black Americans, katika black Americans 10, 7 Ni wajanja wajanja. Naongea kwa experience.

Nimepokea wageni wengi blacks kutoka USA , Hawa jamaa hawana tofauti na sisi wa Buguruni ujanja ujanja mwingi ... Nendeni Zanzibar muulize hili kwa watu wa utalii.


So kuweni makini na Hawa Blacks
IMG_20210611_073537.jpeg
 
Huyu kaacha Deni la zaidi ya laki 7 home maana tuna Hostel za wageni.

Wabongo sio kila anaetoka ng'ambo ana hela wengine Ni njaa. Nina experience Sana na Hawa watu maana home tuna Hostel za wageni ...

Nawaomba muwafuate wamiliki wa hostels za wageniuwaulizie tabia za Black Americans, katika black Americans 10, 7 Ni wajanja wajanja. Naongea kwa experience.

Nimepokea wageni wengi blacks kutoka USA , Hawa jamaa hawana tofauti na sisi wa Buguruni ujanja ujanja mwingi ... Nendeni Zanzibar muulize hili kwa watu wa utalii.


So kuweni makini na Hawa BlacksView attachment 1814889

Kwa hili nitawatetea!! Kiukweli wengi wao wako vizuri tuuu na kati ya watu utaenjoy kufanya nao kazi ni hawa African American!! Maana mimi sijawahi ona watu wajanja janja kama waitaliano ptyuuuuu!!! Nenda Zanzibar alafu fanya comparison
Anyway kila nchi ila wabaya na wazuri lastly
 
Back
Top Bottom