Naomba nijue ubora na udhaifu kati Toyota Kluger na Harrier new model

Babu Kijana

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
584
267
Wakuu habari za leo,

Nina mpango wa kuagiza gari Japan, ninafikiria zaidi Harrier New model au Toyota Kluger za mwaka 2004-2006, nahitaji kujua ubora na udhaifu kati ya hayo magari mawili, na ushauri wa lipi niweze kuagiza.

Pia anaejua kuhusu calculation za mapato TRA na kulitoa gari bandarini, huwa mara nyingi nasikia ile calculator iliyo kwenye website ya TRA huwa inaweza kuwa tofauti kidogo na uhalisia wa gari itakapofika nchini. katika kupita pita websites za magari nimeona bei ya gari na kusafirishwa mpaka tz piga ua inakaa around 5,000 USD.

Nitafurahi kupata ushauri wenu.
 
volgawagen.jpeg
 
1) To be Honest interms of durability/Reality.
Harrier ukifikisha 120km/hr au Zaid inakuwa nyepes sana na inatabia ya kuhama njia mnoo stability inakuwa "0" especialy ukiwa kwenye corner.
Uzur wake gari hii inavutia sana shape yake hasa kwa wakinamama wanaipenda hataree sana.
Ukipakia mzigo mkubwa kwenye boot yake Exel yake ya nyuma inatabia ya Kupinda hivyo tair hulika kwa ndan mpaka urekebishe na ufanye wheel balance

2) kluger hii gari haina sura nzur sana ila ni pana ndan na ukifikisha 120-150km/hr imetulia barabaran utafikir upo 50km/hr inastability nzur sana.

Go for kluger especially durability or go for Harrier if you target physical appearance(gar ya kulia bata mjin haitak usimbufu)
 
Mkuu chukua kluger inaroho ya paka.
 
Babu Kijana ,

Heshima yako!

Nina machache yakudokeza kuhusiana na gari uliyoitaja hapo juu.

Japo hujadadavua haswa ni yenye ukubwa upi wa cc ambao unahitaji
Maana ikumbukwe kwamba, gari hizi zina aina mbili ya engine yaani 6 Cylinders yaani 2,990CC = 3,000CC [3.0]

4 Cylinders yaani 2,290CC = 2,300CC [2.2]

6 Cylinders

ni chache sana ukilinganisha na 4 Cylinders hapa kwetu. Kwa sababu haswa gari hizi ni kwaajili ya watu wa safari ndefu za mara kwa mara, sio gari rafiki sana na safari za ndani (town trips) kwa sababu ina power kubwa na speed vile vile, vitu ambavyo vinachangia utumiaji mkubwa wa mafuta. Kwa wastani, inatembea kilometers 9 kwa Litre. (9KM/L)

4 Cylinders 2,290CC [2.2]

Hizi zipo common sana hapa mjini, na ndio wengi wanazipenda, asilimia kubwa ya hizi ulaji wake wa mafuta hua ni mdogo ukilinganisha na yenye 6 Cylinders kwa wastani hutembea karibia 11 kilometers kwa litre (11km/L)

Haswa hii imelenga kwa matumizi ya ndani (town trips) na sio rafiki sana kwenye kusafiria.

Jambo jingine,

Ambalo nadhani ungepaswa kuelewa ni kwamba, Toyota Harrier na Toyota Kluger ni kitu kimoja.

Yes, ni kitu kimoja, ni kitu kile kile. Unapotaja Toyota Harrier ni sawa unakua umetaja Toyota kluger.

Yaani this is in the sense that it’s only the body design, logo and name that were changed iliku-communicate the difference between the two vehicles.

Otherwise, haya magari (Harrier & kluger) yanatumia almost the same parts na the two engines give the same power output while exhibiting a high fuel consumption regimen.

Hitimisho :

Toyota Harrier na kluger, ni gari ile ile, tofauti kati yake na harrier ipo kwenye muundo wa design.

Na walifanya vile makusudi wakitarajia kwamba, sio wote wangependa muundo wa harrier jinsi ulivyo.

Lakini ukiachilia hapo, Toyota Harrier and Toyota Kluger are actually the same vehicles yenye the same engines type na capacity, the only difference between them being their outward designs.

Otherwise mechanically, and as far as interior design is concerned, you are dealing with the same vehicle.

Kuhusu kikokotozi cha tra,

Kwa Harrier ya 2004

Kwa mujibu wa calculator ya TRA

Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System.

Ni Tzs 11,977,000

Na ya 2006 Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System

Ni Tzs 12,669,000/=

2004 Toyota Kluger, kwa mujibu wa website ya TRA Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System

Ni TZS 10,420,000/=

Na ya 2006 kwa mujibu wa TRA ni Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System

Ni TZS 12,103,000/=

Zingatia :

Unapaswa kuwa na ziada ya angalau TZS 800,000/= Ili iweze ku cover gharama zingine zitakazo ongezeka , pia malipo ya bandarini, shippingline na wakala atakae kutolea gari lako. Itakua humo kwenye hiyo ziada (800,000/=)

Pia kwa sheria mpya ya sasa, gari zote inspection inapaswa kufanyika hapa hapa nchini , hivyo watakutoza pia gharama za inspection.
 
1) To be Honest interms of durability/Reality.
Harrier ukifikisha 120km/hr au Zaid inakuwa nyepes sana na inatabia ya kuhama njia mnoo stability inakuwa "0" especialy ukiwa kwenye corner.
Uzur wake gari hii inavutia sana shape yake hasa kwa wakinamama wanaipenda hataree sana.
Ukipakia mzigo mkubwa kwenye boot yake Exel yake ya nyuma inatabia ya Kupinda hivyo tair hulika kwa ndan mpaka urekebishe na ufanye wheel balance

2) kluger hii gari haina sura nzur sana ila ni pana ndan na ukifikisha 120-150km/hr imetulia barabaran utafikir upo 50km/hr inastability nzur sana.

Go for kluger especially durability or go for Harrier if you target physical appearance(gar ya kulia bata mjin haitak usimbufu)
Hupaswi kamwe kuzungumzia suala la muonekano kwa sabau suala la muonekano hutofautiana kati ya mtu na mtu.Unachokiona wewe kina shepu nzuri kwangu mimi kinaweza kuwa ni shepu mbaya sana.Kwa mfano mimi hakuna shepu ya gari ninayoichukia kama shepu ya Harrier.Lile umbo ambalo watu huwa wanalisifia kuwa ni tako la nyani mimi huwa nalichukia mno!
 
Back
Top Bottom