Naomba nifundishwe kupika ugali wa mahindi

Bakari China

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
251
583
Habari marafiki zangu wapendwa?

Mimi naomba kujua jinsi nitakavyopika ugali wa mahindi, pia mboga zinazofaa (kama vile mchuzi wa nyama au biringani za kukaanga). Mimi ni mpishi mpya, lakini nitajaribu kuzipika vizuri kama iwezekanavyo.

Shukrani
 
Hapana hakuna ugali wa mahindi ndugu yangu labda hayo ni makande.. Pengine ulitaka kumaanisha ugali wa unga wa mahindi, ambao hata hivyo upo wa aina mbili 1. Dona huu unga mahindi yake hayajakobolewa na unatajwa kama unga wenye afya zaidi 2. Sembe.. Huu mahindi yake yamekobolewa. Mapishi yake hayatofautiani sana

MAHITAJI
.Moto (kuni,mkaa, gesi)
.Sufuria/chungu
.Unga wa sembe/dona
.Maji
.Mwiko
.Nyenga/kabari

MAPISHI
Injika chungu/sufuria yako kwenye moto
Weka maji yaache yapate moto kiasi
Weka ungo kidogo kisha ukoroge ushikane vema na maji
Ukishakorogeka ukawa kwenye hatua ya uji acha utokote kwa muda si chini ya dakika 5
Kishapo anza kuongeza unga wako kidogo kidogo huku ukisonga
Unapoanza kuwa mgumu tumia nyenga/kabari kubana sufuria ili usonge vema
Songa kwa kupinduapindua na kuzungusha ukitumia mwiko kwa dakika zisizopungua tano
Ugali tayari . waweza ipua na kuweka kwenye sahani, jani nk ama waweza acha humo humo kulingana na mazingira
 
Hapana hakuna ugali wa mahindi ndugu yangu labda hayo ni makande.. Pengine ulitaka kumaanisha ugali wa unga wa mahindi, ambao hata hivyo upo wa aina mbili 1. Dona huu unga mahindi yake hayajakobolewa na unatajwa kama unga wenye afya zaidi 2. Sembe.. Huu mahindi yake yamekobolewa. Mapishi yake hayatofautiani sana...
asante kwa muongozo wako, unasaidia sana
 
Mimi nashauri tu, mboga ya mchuzi hauta ufurahia ugali wako, tafuta mboga isiyo na mchuzi Mkuu.

Usikose maziwa mtindi/mgando bariiiidi, ukishiba utalala tu
 
Hapana hakuna ugali wa mahindi ndugu yangu labda hayo ni makande.. Pengine ulitaka kumaanisha ugali wa unga wa mahindi, ambao hata hivyo upo wa aina mbili 1. Dona huu unga mahindi yake hayajakobolewa na unatajwa kama unga wenye afya zaidi 2. Sembe.. Huu mahindi yake yamekobolewa. Mapishi yake hayatofautiani sana

MAHITAJI
.Moto (kuni,mkaa, gesi)
.Sufuria/chungu
.Unga wa sembe/dona
.Maji
.Mwiko
.Nyenga/kabari

MAPISHI
Injika chungu/sufuria yako kwenye moto
Weka maji yaache yapate moto kiasi
Weka ungo kidogo kisha ukoroge ushikane vema na maji
Ukishakorogeka ukawa kwenye hatua ya uji acha utokote kwa muda si chini ya dakika 5
Kishapo anza kuongeza unga wako kidogo kidogo huku ukisonga
Unapoanza kuwa mgumu tumia nyenga/kabari kubana sufuria ili usonge vema
Songa kwa kupinduapindua na kuzungusha ukitumia mwiko kwa dakika zisizopungua tano
Ugali tayari . waweza ipua na kuweka kwenye sahani, jani nk ama waweza acha humo humo kulingana na mazingira

Vipimo ni muhimu mkuu mshana.

1---Maji kiasi gani
2---unga kiasi gani
---Unga wa uji kiasi gani kabla ya kuanza kutia unga wa kusongea, kipimo ni muhimu ili mtu asijepika ugali--uji au ugali- jiwe.
 
Duh mshana jr mtu simple Sana ...swali kama la mzaha ila jamaa umeamua kuelezea kabs...uko fresh mkuu
 
Vipimo ni muhimu mkuu mshana.

1---Maji kiasi gani
2---unga kiasi gani
---Unga wa uji kiasi gani kabla ya kuanza kutia unga wa kusongea, kipimo ni muhimu ili mtu asijepika ugali--uji au ugali- jiwe.
Hapo inategemea na wingi wa watu na aina ya ugali mgumu ama laini
 
Mimi nashauri tu, mboga ya mchuzi hauta ufurahia ugali wako, tafuta mboga isiyo na mchuzi Mkuu.

Usikose maziwa mtindi/mgando bariiiidi, ukishiba utalala tu
niliwahi kula ugali mara moja tu, pamoja na mchuzi wa nyama (mboga za kizungu)😅 labda mboga za Kitanzania au Kichina zitanifurahisha zaidi mno
 
Back
Top Bottom