Naomba nifahamishwe kuhusu biashara ya kuuza Pikipiki na Bajaji

Mkuu unaagiza kutoka India/China.MOQ 50PCS wastani wa bei FOB ni kati ya USD 600 hadi USD 2,000 kwa kutegemea na brand na location.Kama Una access ya Milioni 150,000 unaweza kuanza kwa kuwa Custom Bonded Warehouse.Nakutakia Kila la heri.
Samahan mkuu hii mil 150,000 ndio shiling ngap?
 
Mkuu kwanza kwa pikipiki maarufu hapa bongo nazungumzia Tvs na Boxer hizi huwezi kununua india moja kwa moja sababu tayari kuna dealer ambaye ni CAR GENERAL Tz ltd huyu anauza Tvs bike na Tvs king yani kama unataka mzigo unanunua kwake then wewe ndio unauza kwa mtu wa mwisho.

Bei zao kwa jumla bajaji wanauza 7.1M na Tvs bike wanauza 2.2M lakini sasa hizi inategemea kuna 150 na 125 cc bei zinatofautiana. Vigezo na masharti yao wacheki hapo Posta azikiwe ukishuka tu stendi ya daladala.

Kuhusu Boxer ni Mo ndio anasimamia show kwa hapa Bongo wote wananunua kwake. Tembelea ofisi zao zipo K.koo gerezan nafikiri. Mengine watakwambia wenyewe ofisini.

Ila kama una mtaji mkubwa ni biashara nzuri sababu kuna kipindi ziliisha kwa agents wengi hapa dar watu wakawa wananunua kwa dau kubwa zaidi kutoka kwa agents wa mikoani.

Hapo kwa Tvsking (Bajaji) soko ndio kubwa zaidi kwani watu wengi hulipia mzigo kabla hujafika bandarini ukifika wewe unasambaza tu na kuleta mwingine. Nimemaliza
 
Mkuu kwanza kwa pikipiki maarufu hapa bongo nazungumzia Tvs na Boxer hizi huwezi kununua india moja kwa moja sababu tayari kuna dealer ambaye ni CAR GENERAL Tz ltd huyu anauza Tvs bike na Tvs king yani kama unataka mzigo unanunua kwake then wewe ndio unauza kwa mtu wa mwisho. Bei zao kwa jumla bajaji wanauza 7.1M na Tvs bike wanauza 2.2M lakini sasa hizi inategemea kuna 150 na 125 cc bei zinatofautiana. Vigezo na masharti yao wacheki hapo Posta azikiwe ukishuka tu stendi ya daladala.

Kuhusu Boxer ni Mo ndio anasimamia show kwa hapa Bongo wote wananunua kwake. Tembelea ofisi zao zipo K.koo gerezan nafikiri. Mengine watakwambia wenyewe ofisini.
Ila kama una mtaji mkubwa ni biashara nzuri sababu kuna kipindi ziliisha kwa agents wengi hapa dar watu wakawa wananunua kwa dau kubwa zaidi kutoka kwa agents wa mikoani.
Hapo kwa Tvsking (Bajaji) soko ndio kubwa zaidi kwani watu wengi hulipia mzigo kabla hujafika bandarini ukifika wewe unasambaza tu na kuleta mwingine. Nimemaliza
Kwa dhati, nikushukuru ndugu kwa majibu mazuri uliyotupatia.
Ahsante sana.

Jumla, hawa wanataka mtu achukue pc ngapi? Kuna mdau katika kuuliza uliza aliniambia bei ni juu (tofauti ya 200,000) na madukani

Nikashindwa kuelewa
 
Kwa hizi hela wacha nikakaange kuku wa kisasa nipange na kuuza mezani jioni
 
Kama upo dar inatakiwa uingie field mwenyewe kwa hao agents upate machache.

Mitandaoni kuna mislead nyingi sana.

Utakatishwa tamaa.
Upo sahihi mzee , suala ni kwamba hatujawajua hao ma agent ni wangapi na location zao.

Sijui kuna nini , lakini naona watu kama wanajificha sana.
 
Back
Top Bottom