Naomba nifahamishwe kuhusu biashara ya kuuza Pikipiki na Bajaji

Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
507
500
Habari za leo,

Kumekua na thread nyingi zinazohusiana na biashara ya bajaj na pikipiki.

Nyingi zikijikita katika mambo ya uendeshaji wa vyombo hivyo na uuzaji wake wa spare parts.

Lakini sijakutana bado na thread inayoongelea kuhusiana na bei za vyombo hivi (uhakika) maduka vinapouzwa n.k

Hivyo, kwa faida ya wengi, leo ningeomba kuuliza maswali haya machache, kisha nitashukuru kupata mrejesho kutoka kwa wataalamu wanaoelewa

1. Bei ya TVS king (maarufu kama bajaj) pamoja na pikipiki, tvs na boxer ni bei gani?

2. Je, ikiwa mtu anahitaji kufanya biashara ya kuuza vyombo hivi. Taratibu ni zipi za kufuata na wapi anapoweza kwenda kununua mzigo?

Vipi kuhusiana na bei ya huko anapokwenda kununulia mzigo (Bei ya kununulia mzigo) ni kiasi gani na ni maduka gani?

3. Idadi ya pcs unazotakiwa kuchukua ni kiasi gani.?!

Naamini uzi huu utakua msaada kwa wengi, nitashukuru kwa maoni yenu yenye majibu juu ya maswali hayo na hata zaidi.

Nashukuru

1621231024814.png

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,284
2,000
Mkuu unaagiza kutoka India/China.MOQ 50PCS wastani wa bei FOB ni kati ya USD 600 hadi USD 2,000 kwa kutegemea na brand na location. Kama Una access ya Milioni 150,000 unaweza kuanza kwa kuwa Custom Bonded Warehouse. Nakutakia Kila la heri.
 
Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
507
500
Mkuu unaagiza kutoka India/China.MOQ 50PCS wastani wa bei FOB ni kati ya USD 600 hadi USD 2,000 kwa kutegemea na brand na location.Kama Una access ya Milioni 150,000 unaweza kuanza kwa kuwa Custom Bonded Warehouse.Nakutakia Kila la heri.
Ahsante kwa taarifa japo zipo in details

Kuwa bonded warehouse unafanyaje yaani vigeso na masharti yake vikoje ?!
 
Shomary47

Member
Feb 12, 2021
55
125
Mkuu unaagiza kutoka India/China.MOQ 50PCS wastani wa bei FOB ni kati ya USD 600 hadi USD 2,000 kwa kutegemea na brand na location.Kama Una access ya Milioni 150,000 unaweza kuanza kwa kuwa Custom Bonded Warehouse.Nakutakia Kila la heri.
Eleza mkeka vizuri tuelewe
 
Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
507
500
Pesa yako,Masharti yake ni uwe na pesa za kutosha kuwa wakala wa forodha etc.Watembelee Tanzania Revenue Authority - Customs Licenses
Ahsante andoza

Kwahiyo bila kuwa wakala wa forodha
Ni ngumu kufanya importation ya hivi vitu?
Je, kwa hao wanao import na kuuzia wanaotuuzia, je sisi hatuwezi kwenda kununua kwao , na kama ndio

Wanapatikana wapi na bei hua ni kiasi gani.?!
 
andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,284
2,000
Ahsante andoza

Kwahiyo bila kuwa wakala wa forodha
Ni ngumu kufanya importation ya hivi vitu?
Je, kwa hao wanao import na kuuzia wanaotuuzia, je sisi hatuwezi kwenda kununua kwao , na kama ndio

Wanapatikana wapi na bei hua ni kiasi gani.?!
Hapana Hio ni njia ambayo unaweza kuitumia kama ungependa kuwa na Custom Bonded warehouse uweke mzigo mkubwa kabisa.

Unaweza kununua bila shida mzigo wako ukija unalipia kodi unaingiza sokoni unaendelea kuuza.Wauzaji wa Jumla wapo.Cheki na MO ENterprises au Nenda K/Koo wanapatikana watu wanaoagiza in BULK ila tatizo profit Margin Itakukata kama mtaji wako ni mdogo.
 
Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
507
500
Hapana Hio ni njia ambayo unaweza kuitumia kama ungependa kuwa na Custom Bonded warehouse uweke mzigo mkubwa kabisa.

Unaweza kununua bila shida mzigo wako ukija unalipia kodi unaingiza sokoni unaendelea kuuza.Wauzaji wa Jumla wapo.Cheki na MO ENterprises au Nenda K/Koo wanapatikana watu wanaoagiza in BULK ila tatizo profit Margin Itakukata kama mtaji wako ni mdogo.
Andoza,

Nashukuru kwa muda wako pia kwa mawazo unayotoa hapa.

Je kwa hao wauzaji wa kariakoo, ni mtaa gani na bei zao ziko vipi? (Haswa kwa upande wa bajaji ) kwa bei ya jumla.
Na hapo kwa mo, hapa najua watakua ni kwaajili ya pikipiki tuu.. napo bei, zikoje kwa pikipiki zake.?

Ahsante
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom