Rais Magufuli asema haridhishwi na utendaji kazi wa Benki ya Kilimo

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo anazindua Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam muda huu (Juni 04, 2018).

Programu hii ni ya miaka mitano na itagharimu Shilingi Trilioni 13.8

Uzinduzi huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali akiwemo makamu wa Rais na Waziri mkuu.



========

UPDATES:

=> Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi, Reginald Mengi ameomba Serikali iendelee kushirikiana na sekta binafsi kwenye programu ya pili ya kilimo kama awamu iliyopita.

=> Ameahidi kuzindua kitabu chake kinachojulikana kwa jina la I can, I must and I will kitakachoongeza hamasa kwa watanzania

=> Kwa upande wake waziri wa kilimo, Dkt. Charles Tizeba amesema Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa 123% hivyo hatuna tatizo la chakula.

RAIS
=> Rais Magufuli amesema sekta ya kilimo ni muhimu kuhakikisha Usalama wa chakula na ni kichocheo cha kuleta maendeleo ya kiuchumi. Amesema kuna watu wanasema hawapeleki fedha sekta ya kilimo lakini Serikali inazipeleka ila hazitoshi

=> Sisi tangu tulipoingia madarakani tulikuwa tukitenga fedha kwaajili ya Kilimo , Mi huwa nashangaa sana kuna watu wanasema hatupeleki fedha kwenye sekta ya Kilimo, sisi tunapeleka labda kama hazitoshi

=> Tunashika nafasi ya Pili kwa kuwa na mifugo mingi Barani Afrika baada ya Ethiopia, na yawezekana tunawakaribia karibia

=> Sekta ya kilimo hivi sasa inachangia asilimia 100 chakula nchini na asilimia 30 inachangia pato la taifa

=> Kuna siku nilikuwa naangalia TBC, nikaona ghala la Korosho limejengwa kwenye mto, wakati inafahamika korosho haihitaji unyevu. Nilimwambia Waziri wa Kilimo afukuze wahusike siku ile ile na nampongeza Waziri alitekeleza

=> Nguvu kubwa ielekezwe kwenye kilimo cha umwagiliaji, kuna miradi mingi ya umwagiliaji ambayo imetelekezwa

=> Ni ndoto kupata mapinduzi katika kilimo kwa kutegemea mvua tu

=> Chuo Kikuu Sokoine kifanye tafiti nyingi za kilimo na kubuni teknolojia za kisasa, pia kianzishe mashamba ya mifano kote nchini

=> Upo ukweli kwamba muda mwingine fedha zinapotolewa huishia kwenye utawala na hii mifano ipo ambapo serikali inahangaika kutafuta pesa nyingine tunapo kopa hazifikii kwa walengwa zinaishia kwenye shughuli za utawala utaratibu huu usitumike kwenye ASDP2

=> Wasimamizi wa mifuko ya kilimo wahakikishe fedha zinaenda kwenye miradi badala ya kuishia kwenye shughuli za kiutawala

=> Nawakumbusha Mabalozi wa Tanzania walioko nje kuwa moja ya majukumu yao ni kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zetu za kilimo

=> Natoa wito kwa REA na TARURA kuongeza kasi katika ujenzi wa barabara na usambazaji umeme vijijini ili kurahisisha uzalishaji na usafirishaji

=> Naomba niseme ukweli, sijaridhika na utendaji kazi wa Benki ya Kilimo. Benki hii ilianzishwa mwaka 2014 lakini Benki hii inatoa mikopo kwa kusuasua na sifahamu kama Mkuregenzi wa benki hiyo kama anafanya kazi

=> Wakulima wanahangaika hawakopeshwi pesa zao, serikali imekopa. Wangeweza hata kutenga kwamba katika mikoa yote tuliyonayo ni kiasi gani inakopeshwa kwa kila mkoa na tukawapa dhamana wakuu wa Mikoa wakasimamia hiyo mikopo

=> Wizara ya Fedha ihakikishe fedha za Benki ya Kilimo zinakopeshwa kwa wakulima na zisitumike kufanyia biashara na benki nyingine

Habari hii ya Benki ya Kilimo, ilishawahi kujadiliwa hapa JamiiForums, soma=>Rais Magufuli aimulike Benk ya Kilimo, ni hatari
 
Kilimo cha kufa na kupona, siasa ni kilimo, kilimo ni uti wa mgongo,.....lakini kwa maneno tuu hamna utendaji
 
sioni umuhimu wa uzinduzi huuu kufanyika Dar!bado siasa za dana dana zinaendelea kwa wanasiasa dhidi ya Kuliko chetu.ilifaaa program hii izinduliwe mikoani hasa mikoa ya kilimo kama moro na kwingineko.
20180604_092247.png
Museven waters a plant during a heavy rainfall.
 
Kwa hili magufuli nakuunga mkono ila usiishie kwenye kuzindua kwa mikwara mingi ila tunataka tuone kwa vitendo.....

Pambana kwenye kilimo huko ndiko kuna siri ya uzalishaji wa watanzania wengi kutumika na kuongeza pato la taifa achana na maairport ya vijijini na bombardiers pambana kwenye mambo muhim kama haya ndio GDP itapanda kwa kuakisi uhalisia wa maisha ya watanzania
 
Back
Top Bottom