Naomba nafasi yoyote ofisini kwako

Usikate tamaa leo kutokana na hali uliyonayo kwasasa.

Kesho yako ni tofauti na leo yako.

Naomba kutoa mrejesho kama nilivyo ahidi.

Kwanza niseme tu ni ngumu sana MTU kujua kile ulichonacho na kukupa nafasi ilihai hamjuani. Pia kuna watu wana uwezo wa kufanya mengi makubwa na hawapati nafasi au kuchukuliwa poa kutokana na watu kutoelewa kile alichonacho mhusika.

Maisha ni kujifunza na maana halisi ya maisha ni mkusanyiko wa experiences tofautitofauti ambazo huwa na ups and downs. Wengi hatuna MATATIZO ila tuna CHANGAMOTO ambazo zinahitaji muda na utulivu kutafutia ufumbuzi ili maisha yaweze kusonga, hivyo katika maisha yako usije wahi jitamkia umesongwa na MATATIZO, hapana sema nina CHANGAMOTO ambazo zinahitaji ufumbuzi hivyo muda na utulivu katika kutafuta suluhisho ndio njia pekee unayohitaji kutumia.

Bandiko langu la kuomba nafasi ya kazi mpaka sasa sijapata kazi japo kuna appointments kadhaa ambazo nilizipata kutoka kwa member. Na kutokana na changamoto ambazo zilikuwa nje ya uwezo kwa pande zote mbili ilibidi kupeana muda ili muda wowote niweze kuanza.

Bado niliitaji maisha yaweze kuendelea wakati nasubiri mambo hayo kukaa sawa hivyo nilikuwa na jukumu la kuendelea kutafuta shughuli za kuingiza kipato kukidhi mahitaji ya hapa na pale.

Kazi za saidia fundi nimepiga zimenisaidia kusukuma maisha mpaka kupata kile kiasi ambacho nilikuwa nakilenga ili kuanzisha ofisi ndogo ya kuanzia kutokana na uzoefu wangu hapo juu kwenye mada kuu na pia vitu vingine ambavyo navielewa.

Namshukuru Mungu kwasababu haikuwa rahisi lakini nilipata ujasiri na kufanya na kufikia lengo japo la KUANZA tu!.

Kwasasa Mungu ni mwema, mambo siyo magumu kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa wale wenzangu ambao hali ni ngumu na wameweka mabandiko humu ya kutafuta kazi, naomba kusema mabadiliko ya maisha yako yanaanzia kwako mwenyewe ndipo matokeo yanaonekana nje, JF ilikuwa ni last option kwangu maana niliona mambo yanazidi kukaza lakini bado kichwani nilikuwa na PLAN B, in case kama bandiko la JF lisingeleta matokeo yoyote.

Nini maana ya kusema hayo, lazima katika maisha uwe na plan zaidi ya moja hasa wakati wa changamoto maana kwa njia hiyo ni rahisi kupata suluhisho katika moja ya plans ulizoweka.

Haya mambo siyo rahisi kama ninavyoeleza ila huu ni muongozo tu wa wewe kuingia vitani. Waliofanya kazi za saidia fundi nadhani wanaelewa ugumu na changamoto za kazi hii. Mwanzo kwa siku niliweza kukaa na computer yangu na kuingiza 10k-50k kwa siku na sometimes hadi 100k kwa siku, na niliporudi kufanya kazi ya saidia fundi nalipwa 15k kwa siku, kazi ngumu, matusi humohumo, na muda unatumia siku nzima unafika nyumbani umechoka mwili wote umelegea, nilitamani kuacha siku ya kwanza maana nilichubuka mabega kutokana na kubeba vitu vizito kwa muda mrefu, na mikono miguu dah! Ilikuwa ni Changamoto sana.

Ila nilikaa nikakumbuka lengo langu kuu naona hamna namna ni lazima nipambane kutimiza lengo kwasababu sina namna nyingine zaidi ya kukomaa.

Kitu kilichonisaidia ni uwezo wa kuwa na FIKRA CHANYA katika nyakati zile ngumu. Niliamini ni fursa ambayo ipo kunifungua fikra na kunipandisha daraja.

Hivyo ewe ndugu yangu na kijana mwenzangu ambaye bado unaona mambo magumu, neno Never give up, maana yake ya kwanza ni kubadili namna ya kufikiri kwako. Wajibika, beba mzigo wako na njiani wapo wasamaria watakusaidia kubeba huo mzigo na utafika.

Pambana, jenga mtazamo chanya, usikate tamaa, inawezekan ukiamua.

Zaidi ya yote jifunze kuwa na malengo katika maisha. Ijue siku yako, wiki yako, mwezi wako, mwaka wako, miaka mitano yako, miaka 10 yako na miaka 50 yako IJAYO, unategemea kufanya nini, wapi na kwa nini?.

Asanteni kwa wote milonitia moyo na Mungu azidi wabariki.
 
Habari wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 24, nipo Dar es salaam, Kurasini maeneo ya uhasibu.

Nipo hapa leo kuomba nafasi ya kazi yoyote kulingana na uzoefu wangu huu.

1. Nimefanya kazi ya stationery, nina uzoefu sana upande wa kazi za internet cafe, zile online applications za aina mbalimbali nafanya.

2. Nimefanya kazi za kutengeneza social media accounts mbalimbali kwaajili ya biashara, yaani kutengeneza Facebook accounts, sponsored ads za Facebook na Instagram, kutengeneza blogs, kutengeneza channel za YouTube.

(Kiujumla naweza fanya digital marketing)

3. Pia nina ujuzi mzuri wa computer.

4. Nimefundisha physics na mathematics kuanzia form one hadi six. (Nipo vizuri sana kwenye masomo ya mathematic)

5. Ni mbunifu hasa katika kufanya biashara na kuongeza thamani katika biashara husika.

6. Nina uwezo wa kutengeneza maudhui katika social media accounts, blogs au websites pia (nimefanya blogging pia ni msomaji mzuri wa vitabu mbalimbali)

7. Ni muandaaji mzuri wa vitini vya masomo ya physics, chemistry na mathematics (nimefanya kazi na baadhi ya wamiliki wa apps na blogs za elimu).

8. Kusimamia miradi na biashara ( nina uzoefu hasa katika kusimamia masuala ya ujenzi)

9. Kiafya niko vizuri na hata kazi za kutumia nguvu pia nafanya.

Kuna ofisi nilikuwa nafanyia kazi ila mmiliki alihama kutokana na changamoto za kifamilia December 2020, hivyo kwasasa nimeona nitafute shughuli yoyote walau kuendesha maisha wakati najipanga kuandaa ofisi yangu rasmi.

Elimu yangu nimefika chuo, ila kutokana na Changamoto za kijamii na uchumi nilisoma hadi mwaka wa tatu na sikuweza kuendelea.

Mimi ni mtu mwenye malengo katika maisha na hii kazi naomba ili kuendelea kupanua uelewa wangu zaidi na kupata uzoefu kiujumla na kuendesha maish kwa muda huu ambao najipanga ili kuanza kufanyia kazi ndoto zangu.

Pia kwa yeyote mwenye maswali, ushauri pia ntashukuru kupata mungozo.

Mungu awabariki wote mtakaoguswa katika hili.
 
Usikate tamaa leo kutokana na hali uliyonayo kwasasa.

Kesho yako ni tofauti na leo yako.

Naomba kutoa mrejesho kama nilivyo ahidi.

Kwanza niseme tu ni ngumu sana MTU kujua kile ulichonacho na kukupa nafasi ilihai hamjuani. Pia kuna watu wana uwezo wa kufanya mengi makubwa na hawapati nafasi au kuchukuliwa poa kutokana na watu kutoelewa kile alichonacho mhusika.

Maisha ni kujifunza na maana halisi ya maisha ni mkusanyiko wa experiences tofautitofauti ambazo huwa na ups and downs. Wengi hatuna MATATIZO ila tuna CHANGAMOTO ambazo zinahitaji muda na utulivu kutafutia ufumbuzi ili maisha yaweze kusonga, hivyo katika maisha yako usije wahi jitamkia umesongwa na MATATIZO, hapana sema nina CHANGAMOTO ambazo zinahitaji ufumbuzi hivyo muda na utulivu katika kutafuta suluhisho ndio njia pekee unayohitaji kutumia.

Bandiko langu la kuomba nafasi ya kazi mpaka sasa sijapata kazi japo kuna appointments kadhaa ambazo nilizipata kutoka kwa member. Na kutokana na changamoto ambazo zilikuwa nje ya uwezo kwa pande zote mbili ilibidi kupeana muda ili muda wowote niweze kuanza.

Bado niliitaji maisha yaweze kuendelea wakati nasubiri mambo hayo kukaa sawa hivyo nilikuwa na jukumu la kuendelea kutafuta shughuli za kuingiza kipato kukidhi mahitaji ya hapa na pale.

Kazi za saidia fundi nimepiga zimenisaidia kusukuma maisha mpaka kupata kile kiasi ambacho nilikuwa nakilenga ili kuanzisha ofisi ndogo ya kuanzia kutokana na uzoefu wangu hapo juu kwenye mada kuu na pia vitu vingine ambavyo navielewa.

Namshukuru Mungu kwasababu haikuwa rahisi lakini nilipata ujasiri na kufanya na kufikia lengo japo la KUANZA tu!.

Kwasasa Mungu ni mwema, mambo siyo magumu kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa wale wenzangu ambao hali ni ngumu na wameweka mabandiko humu ya kutafuta kazi, naomba kusema mabadiliko ya maisha yako yanaanzia kwako mwenyewe ndipo matokeo yanaonekana nje, JF ilikuwa ni last option kwangu maana niliona mambo yanazidi kukaza lakini bado kichwani nilikuwa na PLAN B, in case kama bandiko la JF lisingeleta matokeo yoyote.

Nini maana ya kusema hayo, lazima katika maisha uwe na plan zaidi ya moja hasa wakati wa changamoto maana kwa njia hiyo ni rahisi kupata suluhisho katika moja ya plans ulizoweka.

Haya mambo siyo rahisi kama ninavyoeleza ila huu ni muongozo tu wa wewe kuingia vitani. Waliofanya kazi za saidia fundi nadhani wanaelewa ugumu na changamoto za kazi hii. Mwanzo kwa siku niliweza kukaa na computer yangu na kuingiza 10k-50k kwa siku na sometimes hadi 100k kwa siku, na niliporudi kufanya kazi ya saidia fundi nalipwa 15k kwa siku, kazi ngumu, matusi humohumo, na muda unatumia siku nzima unafika nyumbani umechoka mwili wote umelegea, nilitamani kuacha siku ya kwanza maana nilichubuka mabega kutokana na kubeba vitu vizito kwa muda mrefu, na mikono miguu dah! Ilikuwa ni Changamoto sana.

Ila nilikaa nikakumbuka lengo langu kuu naona hamna namna ni lazima nipambane kutimiza lengo kwasababu sina namna nyingine zaidi ya kukomaa.

Kitu kilichonisaidia ni uwezo wa kuwa na FIKRA CHANYA katika nyakati zile ngumu. Niliamini ni fursa ambayo ipo kunifungua fikra na kunipandisha daraja.

Hivyo ewe ndugu yangu na kijana mwenzangu ambaye bado unaona mambo magumu, neno Never give up, maana yake ya kwanza ni kubadili namna ya kufikiri kwako. Wajibika, beba mzigo wako na njiani wapo wasamaria watakusaidia kubeba huo mzigo na utafika.

Pambana, jenga mtazamo chanya, usikate tamaa, inawezekan ukiamua.

Zaidi ya yote jifunze kuwa na malengo katika maisha. Ijue siku yako, wiki yako, mwezi wako, mwaka wako, miaka mitano yako, miaka 10 yako na miaka 50 yako IJAYO, unategemea kufanya nini, wapi na kwa nini?.

Asanteni kwa wote milonitia moyo na Mungu azidi wabariki.
Ushauri tumeupokea.
 
Ni kweli mkuu. Siyo fani. Ila target yangu ni kufanya shughuli zenye kuhitaji ujuzi wa computer.

Napenda masuala ya online.

1. Digital markets kiujumla (kuna vipengele bado najifunza mpka sasa kam web design hasa hizi e-commerce websites)

2. Online application za aina zote (ulimwengu unaamia mtandaoni mkuu, leo tunakata tiketi za basi on-lin)

Kiujumla nalenga shughuli za mtandaoni na mambo ya computer kwa kufanya na kufundisha pia.

Napenda na ina faida sana maana nimeshaifanya.

Kumiliki apps na website pia.

Kiujumla kwasasa natafuta backup walau nipate kazi ambayo itanisaidia kwa muda huu ambao nipo tu na mtaji wa kuanzisha ofisi yangu rasmi bado sina.

Kiufupi nina mengi sana mkuu zaidi ya hayo niliyoyaeleza.
Umesema unajua hesabu na physics na unapenda shuguli za online.

Sasa sikiliza. Anza kujifunza web developing, umalize, kisha uhamie programming, (hapa usomee kila kitu kinachohusiana na Android Studio) C++ na hata python, kama utaweza,

Ukishaweza kuandaa app, tukae chini, nikupe mchongo, tufanye then tugawane profit 50-50.

Mi nitafanya marketing na kutafuta investment.

Profit tunasplit after matumizi yote. Nicheki DM tuyajenge zaidi.
 
Shukrani sana mkuu kwa mawazo mazuri boss. Ntakucheki mkuu
 
Back
Top Bottom