Naomba mwongozo. Serikali ya mseto bara inawezekana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mwongozo. Serikali ya mseto bara inawezekana?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Raia Fulani, Nov 22, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna mdau kaniambia katika majadiliano kuwa mseto hauwezekani bara kwa vile chama chenye wabunge wengi ndicho kinaunda serikali. Sasa pamoja na hayo chama tawala hakina mamlaka kuteua mawaziri toka upinzani kisa wana viti vingi au sheria inawabana?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kinadharia mseto unawezekana. Kama rais anayeshinda atakuwa hana wabunge wengi atalazimika kuchagua waziri mkuu kutoka chama chenye wabunge wengi. Huo ni mseto tayari. Rais ana uwezo wa kuteua mawaziri kutoka upinzani, inaruhusiwa.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Inawezekana wala kikatiba haizuiliwi!
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa suala la waziri mkuu nafaham hivyo ulivyoeleza. Inakuwaje kama akitaka kuteua waziri let say wa fedha toka upinzani. Katiba inamruhusu?
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rais anaweza kumteua mbunge yeyote yule kuwa waziri. Katiba inaruhusu.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hapana, serikali ya mseto inaondoa demokrasia kabisa. Kama vyama vyote vitaunda serikali ya mseto then kutakuwa hakuna upinzani na tutakuwa tumerudia mfumo wa chama kimoja chenye matawi tofauti. Serikali ya kitaifa lakini siyo ya mseto. Kujenga kwa serikali ya kitaifa kunawezekana iwapo tutakuwa na utaratbu mzuri sana wa kutenganisha mambo ya serikali na mambo ya siasa. Yaani serikali na vyombo vyake visijihusihe moja kwa moja na kampeini zozote za kisiasa. Waziri asitumie nafasi ya uwaziri kupiga debe la kisiasa. Chini ya utaratibu huo, inawezekana chama chenye serikali kuhusisha baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani kwenye serikali yake kama ambavyo Marekani wanafanya. Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Klintoni alikuwa ni Republican william Cohen, Waziri wa uasfirishaji katika serikali ya Bush alikuwa Norman Y. Mineta ambaye ni Democrat, na sasa serikali ya Obama ina William Gates ambaye ni Waziri wa Ulinzi akiwa ni Republican.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nashukuruni kwa maoni wadau. Kama alivyosema kichuguu hapo juu, kibongobongo ni ngumu kuwa na serikali ya mseto japo haijakatazwa kikatiba
   
 8. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mawaziri wanachaguliwa kwa ridhaa ya Rais bila kujali chama, ye tuu ndo anaamua, nani wa kumchagua. Ila ningekua Kikwete nampa uwaziri John Shibuda na Zitto Kabwe tuone kama CHADEMA itakubali huo uteuzi au itawavua uanachama. Siasa si chuki ni kama mchezo wa karata
   
 9. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kabla ya kuongelea kama serikali ya mseto au vinginevyo kwanza tujiulize kuna serikali ya bara?
  Swali liko wazi kabisa kama inawezekana serikali ya mseto bara. Kwanza uwepo uwezekano kikatiba wa kuwapo serikali ya bara, halafu tuone inakuwa ya muundo upi.
   
 10. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Agenda ya siis ya mfumo wa serikali za mseto ni kuua demokrasi kabisaaaaa!!!!!!!!!!! Hebu niambie ZBR bado kuna ushindani wa upinzani?? Nani atamnyooshea nani kidole??????? Katika bunge letu la sasa hata kabla ya vikao kuanza kafu kwa kujiunga na sisiemu moto wa upinzani tayari opposition imebaki CDM tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Niambie nchi gani dunuani zilizoendelea zinafuata mfumo huu????????? This is mugabe/kibaki style!!! Kibaki yeye wajanja walimwahi na kumzima kwa katiba mpya ambayo tayari imemtupa nje!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mugabe yeye anapeta lakini kwa mauti ya taifa la Zimbabwe kiuchumi na kijamii!!!!!!!!!!!!!!! Masikin Zimbabwe!!!!!!!!!-once Southern Rhodesia ambayo kwa nguvu ya uchumi ilikuwa second to Bondeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...