Naomba mwongozo kuhusu makamu wa pili wa rais wa Zanzibar- Balozi SEIF ni mbunge....?

Ras Cutty

Member
Nov 12, 2010
42
10
Wadau wa JF ambao mnelewa mtueleweshe hivi huyu Balozi SEIF ambae ni makamu wa pili wa rais wa Zanzibar yeye ni mbunge wa bunge lipi?? maana ameteuliwa kuwa mbunge wa baraza la wawakilishi na tena juzi tumemuona akiwa anaapa kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano kule mjengoni. wengine hatujaelewa hapo. Hivyo twaomba wadau wenye data au majibu ya hilo watuelimishe imekuaje au ndio mabadiliko ya katiba ya zenji au vipi??????:israel:
 
Aisee katiba ya Zenji hata mimi huwa siielewi elewi.
Mara makamo wa raisi aapishwe na raisi mara makamo wawili wa rais ktk nchi moja! Tabu tupu!
 
hata m hapo naona kuna mkanganyiko kidogo make ni mbunge katika JMT na ni makamu wa rais.Tunaombwa tufahamishwr hapo muundo unakuwaje.
 
Balozi seif ali iddi ni mbunge jmt wa kuchaguliwa na wananchi ktk jimbo la kitope unguja lkn pia ni mwakilishi wa kuteuliwa na rais wa znz ambae pia amemteua kua makamo wa pili wa smz. Sheria haimzui mtu kua mwakilishi znz halafu akawa mbunge wa muungano. Watu kama hao wapo eg asaa ni mwakilishi wa wete lkn pia ni mbunge wa muungano kama vipi tuvunje muungano basi au?
 
Wadau wa JF ambao mnelewa mtueleweshe hivi huyu Balozi SEIF ambae ni makamu wa pili wa rais wa Zanzibar yeye ni mbunge wa bunge lipi?? maana ameteuliwa kuwa mbunge wa baraza la wawakilishi na tena juzi tumemuona akiwa anaapa kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano kule mjengoni. wengine hatujaelewa hapo. Hivyo twaomba wadau wenye data au majibu ya hilo watuelimishe imekuaje au ndio mabadiliko ya katiba ya zenji au vipi??????:israel:
Balozi SEIF Iddi ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la kitope Unguja ,Zanzibar.... Ameteuliwa tena na Rais wa Zanzibar kuwa muwakilishi wa kuteuliwa na Rais, ili baadae amchague awe Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar, ili mtu awe katika baraza la mawari la Zanzibar, lazima awe muwakilishi hata kama wakuteuliwa na Rais...kwani rais anayo haki ya kuteuwa wawakilishi 10 ambao hawakupigiwa kura na wananchi...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom