Naomba muongozo wa kuwa wakala wa makampuni ya bima

radicals

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
4,412
6,447
Habari za wakati huu wanajamvi

Nashukuru sana kwa ushauri mlionipa pia ningeomba mnivumilie kwa post zangu mfululizo za aina hii. Kuna uzi niliutoa jana kuhusu locations za maeneo ya biashara ya uwakala m pesa, tigo pesa, benk, nk;

Katika kutembelea sehemu tofauti mlizoni direct, nmeipata my dream location na nikijaaliwa leo ndio nitakuwa nalipia, dalali aliyenionesha fremu hiyo kanishauri niongezee na uwakala wa BIMA, kwani watu wa eneo hilo wanapata shida sana, insurance agents wapo mbali sana, nami nikaona hii ni fursa,,,

Sasa kwenu wadau nauliza hivi
(1) Je ni taratibu zipi nazotakiwa nifuate ili niwe wakala wa insurance companies

(2) Je miamala ya insurance ipo vipi, na commission wanalipaje

(3) pia mtaji niwe nao minimum kiasi gani?


NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU ZA DHATI, KARIBUNI MCHANGIE
 
Back
Top Bottom