Naomba muongozo wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba muongozo wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sam, May 30, 2008.

 1. S

  Sam JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa lengo la kwanza la CHADEMA wakiingia madarakani ni kuitisha mkutano wa Katiba sasa na kwa matazamo wangu nadhani kama hilo ni lengo wa kwanza basi CHADEMA haina sera kwa sasa. Kwa nini nasema hivyo, kwa mfano wananchi wakikataa mfumo wa majimbo kwenye katiba ni kivipi CHADEMA itatekeleza mfumo huo na kwa vile CHADEMA inaamini kuwa huo mfumo utatuletea maendeleo ya haraka sasa ni kivipi itatuletea maendeleo bila mfumo huo? Navyojua mimi sera za vyama vinatokana na katiba iliyopo. Kwenye sera ya utawala CHADEMA wamesema watapunguza mikoa kuwa 10 sasa kama katiba itakayoundwa itasema rais/chama hakitakuwa na mamlaka ya kugawa mikoa, je CHADEMA itakumia udikteta kuunda mikoa 10? Naomba muongozo.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Thread nzuri sana hii,
  Viongozi na wanachama wa chadema wamekuwa wakikimbia kujibu maswali ya msingi!
  Naomba pia ikumbukwe kuwa katika huo mfumo wa majimbo mojawapo ya wanachotaka kufanya ni kuondoa cheo cha Rais wa Zanzibar.
  Je ni muda gani wenzetu hawa wanahitaji ili waweze kuunda serikali baada ya kushinda uchaguzi??? Serikali ambayo wanaamini ndio itakayoweza kuleta mapinduzi ya uchumi!!!
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kumbukeni kuwa CHADEMA kinaamini kwenye uwepo wa serikali tatu yaani ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya muungano , hivyo swali juu ya Zanzibar halipo hapo.

  Pili kuhusu kutaka muongozo , ni kwanini mtoa mada aamini kuwa wananchi watakataa mfumo wa serikali ya majimbo, nenda kasome ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005 utapata majibu ya maswasli yako yote pamoja na muda uliokuwa umehitajika kutekeleza jambo hilo.

  Ingia www.chadema.net tafuta ilani ya uchaguzi hutarudi kuja kuongeza kujaza nafasi hapa na maswali kama haya.

  Nawatakia msome kwa undani na kuelewa.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Maelezo aliyoyatoa Zitto hapa JF akimjibu Rev. Kishoka yanapingana na unachosema hapa. Alisema kuwa Rais wa Zanzibar atatolewa halafu kutakuwa na waziri mkuu wa Unguja na wa Pemba.

  Ukihitaji quote yote nitakuletea. Au unaweza kuipata kwenye thread ya "CHADEMA waanzisha mjadala wa sera ya majimbo".
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  CHADEMA kwa ujumla kimekuwa ni chama ambacho kila kiongozi anashikilia sera zake mwenyewe! tukumbuke jinsi wabunge wote wa upinzani walivyogoma kupinga kitendo cha kutokupitishwa kwa muafaka wa Zanzibar ambapo CCM walishauri kuwe na kura za maoni.Wiki chache baadae akatoea Chacha Wangwe, kupinga kuwepo kwa serikali ya Umoja huko Zanzibar. Inakuwa vigumu kuelewa nini kilimfanya agomee Bunge kama anapinga serikali ya umoja Zanzibar!

  Wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa kama CHADEMA ni chama au ni nyenzo tu inayotumiwa na watu kujisajili ili waweze kufanya mambo yao ya kisiasa kama independents kitu ambacho wangeshindwa kukifanya kwa sababu bado hakijapitishwa!
   
 6. S

  Sam JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani CHADEMA mpo? Mbona sijapata majibu. Zitto vipi?
   
 7. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hapa patamu leo !
  !
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mwanzo wa Ngoma lele
  naamini ktk mijadala kama hii chama badala ya kujitetea waje na majibu makini ili kujenga uwezo wa kuaminika na sisi wenye kura.

  Ni kweli CCM waberonga tena kwa kiwango cha kutisha ila wameboronga zaidi kwa kuanzisha vyama pandikizi ili kuua upinzani, kwa chama makini huu ndio wakati wa kujenga msingi wa uwezo wa kuaminika kwa wananchi wengi. Kama CCM wana miradi na walikuwa na ile kitu inaitwa Biashara Consumers Limited kwa nini hivi vyama wasije hata na mashamba ya mifano ambayo kwayo watahubiri mapinduzi ya kilimo, kwa nini wasije na kitu kitakachotoa taswira ya kuweza kubeba dhamana??

  Kila mpinzania ni mtanzania mwenzetu ambaye naamini kila aliwazalo ni kwa maslahi ya Taifa. Mfano mzuri ni Nyerere na Slaa....

  Chadema leteni hoja na siyo hadithi za sungura hapa
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado sijakiona chama makini cha kuweza kukiondoa CCM madarakani mpaka sasa
  waliopo ni wababaishaji na waganga njaa tu
   
 10. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inategemea vision yako ikoje... ukiwa fisadi huwezi kuona hili!
   
 11. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe mdada sijui mkaka kazi kwelikweli
  hivi mtu akiwa na mawazo tofauti na upinzani tu basi keshakuwa fisadi?
   
 12. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtu yeyote anayetetea ufisadi ni fisadi.. what about that!
   
 13. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa wapi mimi nilipotetea fisadi?au nilivyosema ukweli kuhusu wapinzani uchwara wa tanzania basi ndiyo nimeshakuwa fisadi?
  wewe fikiria mtu kama prof shayo nae eti anagombea urais.yaani mtu anajua kabisa hata mkewe asingeweza kumpa kura lakini nae anakwenda kuchukua fomu.mtu anajua kabisa hata akigombea udiwani kwao bado inaweza kuwa mbinde kuupata,halafu anagombea urais.kama siyo ubabaishaji nini sasa?tukisema mnatuita mafisadi.Hili neno la fisadi sasa naona limekuwa kama pipi mdomoni
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna ushauri umepewa kwamba ukasome nini ya mwaka 2005.Je umesha soma ama hutaki hadi aje Zitto hapa aseme ndipo uelewe ?

  Kada Mpinzani kumbe upo nilidhani umekufa , ikisemwa Chadema tu unatokeza ? Shame on you hata hoja huwezi kujenga ila ushabiki ?

  Again mmepewa habari na link iko hapo juu kasomeni then mrudi na majibu yenu baada ya kusoma .
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hayo ya Prof Shayo sina comment.. ila hayo ya kusema kuwa hakuna wa kuitoa ccm kwa miongo kibao ijayo (paraph..) ninapingana nayo. kuhusu wewe kuwa fisadi, ukisoma post yangu vizuri utagundua kuwa nimetoa conditional statement..

  Labda niiweke tena hapa ili ujue kuwa sikukuita wewe fisadi:

   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtarajiwa , kindly elaborate kwamba hujaona Chama mbadala zaidi ya CCM .Kuna nini ambacho kipo CCM ambacho huwezi kukipata katika Upinzani ? Najua yako mengi kwa mfano ufisadi , kufisadi kura, kutumia vibaya madaraka nk .Haya ni kweli Upinzani hayako ila yako CCM.Nieleze mengine tafadhali .
   
 17. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Lunyungu kitu gani kimekufanya uhisi kuwa mimi ni ccm?Mimi sijasema kwamba ni CCM wala CUF wala DP au CHADEMA,nimetoa mtazamo wangu tu kuhusu upinzani wa tanzania.maovu ya ccm yanajulikana na kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na tanzania na watanzania angependa kuona kweli watanzania wanapata wapinzani makini kama mbadala wa CCM ama kuwang'oa ccm ama kuwafanya wabadirike.sasa hili ndilo ninalolizungumzia mimi kuwa kwa sasa tanzania chama hicho hakipo bado.
  Labda tumshukuru Mtikila kutuletea wagombea binafsi basi!
   
 18. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtarajiwa,

  hiki ndicho uliandika kabla huja-edit post yako:

   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtarajiwa I never call people names.Mimi huwa najadili nikiwa nina la kusema .Nikiwa sina nakaa kimya .Sijakuita wewe CCM ila soma tena uone nimeongea nini .Utofauti wa mawazo unatakiwa ili kuwa na kitu kincho eleweka .Lakini wewe unamchukua Prof SAhayo unamtukana nakusema Wapinzani.

  Wapinzani wakisema Rostam Mwizi so CCM ni wezi wanasema no just single out the person . Vipi hapa sisi Watanzania ?

  Kuna mapandikizi yanajulikana na jukumu la vyama vyenye mwelekeo nakukubalika kuwa makini lakini kusema Wapinzani wana njaa nk ni chuki na inakupunguzia heshima .

  Kuna mtu majuzi kasema JF ni kijiwe cha kijinga maeno ya Kariakoo walitaka kumezwa ikabidi nianze usuluhuishi .Ila CCM wanasema sisi ni Kijiwe na baadhi yao kama Kilango Mwakyembe ukiwauliza juu ya JF hata JK anajua tuna nondo kali .Nimekupa mfano tu ili usione nimekuvaa hapana .Nataja ujibu maswali yangu sasa hapo juu tafadhali .
   
 20. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa mwkike huo ndiyo uthibitisho kwamba mimi ccm???
  mnajua tusiongee kiushabiki jamani ccm imejichimbia.nendeni vivijini ndiyo mtajua ccm nani na hao ndiyo wapiga kura wenyewe..
  ndiyo mana mimi nilishaanzisha thread hapa,hawa kina mbowe,lipumba,mrema,mbatia,prof.baregu nk nk, kwanini kwanza wasianze kugombea ubunge ili waongeze nguvu kule?why urais in the first place hali wakijua wazi kuwa hawatashinda??
   
Loading...