Uchaguzi 2020 Naomba Mungu uchaguzi upite shughuli ziendelee

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Inakera sana tena sana,sasa hivi kila mwananchi anakosa huduma za msingi, kisa tu uchaguzi na kampeni.

Ukienda kwa wakuu wa Wiaya, Wakurugenzi na hata Watumishi wa afya watakuambia wapo bize na shughuli za serikali.

Swali la msingi je serikali imesimama kufanya kazi kisa tu uchaguzi na kampeni? Mbona tunanyanyasika kwa uchaguzi ambao hata matokeo yaliyashapangwa?
 
KUNA HAJA YA WATU KAMA MUSIBA KUPIMWA AKILI HII SASA SIO SIASA NI SHAMBULIO BINAFSI
 
Inakera sana tena sana, sasa hivi kila mwananchi anakosa huduma za msingi, kisa tu uchaguzi na kampeni .

Ukienda kwa wakuu wa Wiaya, Wakurugenzi na hata watumishi wa afya watakuambia wapo bize na shughuli za serikali.

Swali la msingi je serikali imesimama kufanya kazi kisa tu uchaguzi na kampeni? Mbona tunanyanyasika kwa uchaguzi ambao hata matokeo yaliyashapangwa?
wapi kazi zimesimama mkuu?
 
Baada ya uchaguzi ndio shughuli inaanza,

Hii nchi haitakaa iwe kama ilivyokuwa kabla ya uchaguzi bila kujalisha atakayeshinda uchaguzi.
 
Tuna haki ya kutoa maoni yetu binafsi lakini unapousemea umma unakosea mkuu,maisha yamesimama kwako kutokana na ubinafsi wako maadam wewe umeshiba na familia yako hujui ya jirani yako kama nayo imeshiba,serikali bado na haijalala sasa hizo shughuli zilizosimama zipo wapi?acha kuzamisha kichwa chako mchangani amka and smell the coffee
 
Back
Top Bottom