Naomba msamaha kwa Siasa zangu chafu na Propaganda

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,357
2,000
Wanabodi, Kuomba msamaha sio ujinga bali ni kujitakasa mbele za Muumba.

Napenda kutumia nafasi hii kuomba msamaha kwa wote niliowakosea kwa kujibu hovyo au kutukana Katika thread zangu, Reply Back na Comments zangu.

Nimeomba radhi baada ya kujifunza jinsi kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu Hayati Rais wetu afariki dunia na kabla hata nguo hazijaoza jinsi wanaobaki wanakusuta, wanakusema na kuongea ubaya wako wote wa uliyoyafanya hapa Duniani.

Hakika nimechukua mitazamo mipya sana na kuamua kuacha baadhi ya Propaganda pembeni ambazo zilikuwa zinakwaza na kuumiza Wengine huku nikijua sio sahihi nifanyacho kwa taaluma yangu na weledi wangu. Zaidi ya hapo wazazi wangu hawakunilea hivyo kuwa mtu wa kupiga Propaganda wakati maelfu wanaumia.

Nina mazuri yangu mengi hapa JF ambayo niliamua kutumia akili zangu na mchango wangu vizuri hayo nitayaendeleza kwa weledi na taaluma yangu.

Propaganda zote nilizozifanya hapa JF kwa miaka mitano za kusifia pale palipoharibika ninaomba msamaha kwa niliowakwaza.

Kwa Imani yangu Mimi huwezi kwenda mbele bila toba na kuyaorodhesha baadhi ya mambo niliyoyafanya kwa Propaganda huku nikijua ni uwongo.

Mosi, Kusifia ajira kwa vijana huku nikijua vijana wana hali ngumu.

Pili, Propaganda za mishahara kwa watumishi kuwa wasiongezwe bali iendane na Uchumi huku nikijua ni haki yao ya msingi.

Tatu, Kumjibu mtu vibaya kwa kugusa Personalities zake Baba yake, Mama yake au Familia yake badala ya kujibu hoja yake. Hili limeniumiza sana na ninaomba msamaha sana.

Mwisho, Tuishi kwa upendo na Amani, Tuongee yaliyo kweli daima kwa maslahi ya Taifa letu.

Tuishi vizuri ili watu wasimulie mema yetu lakini si kwa kusimulia maovu na ubaya wetu, Tuombe msamaha pale tunapokosea.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,667
2,000
Mkuu kwenye hiyo namba 2 ulinikwaza sana mkuu jinsi ulivyokuwa unapiga porojo wakati sisi tukiumia! Mpaka wengine tumeamua kuachia ngazi huko serikalini na kurudi kwenye NGOs lakini wewe ulikuwa unaona sawa tu!

Mkuu kwa vile umetubu mimi binafsi nimekusamehe ingawa ulikuwa nyoko sana!

Magufuli yeye hakupata fursa hata ya kutuomba msamaha kwa hiyo amekufa na donge letu! Bora wewe umelitambua hilo, sasa kazi iliyobaki pia uende mbele ya Sheikh au Padre utubu pia!
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,357
2,000
Duh, sasa ulifanya vile kwa malengo yapi? unadhani kwa siasa za mtindo ule nchi yetu itasogea kweli? hiyo tabia mwambie na Ndugai aiache kule bungeni.
Kiongozi, Ni kukosa utu na ubinadamu tu, Na ni ile hali ya kujiona maisha unayoishi wewe ni wewe tu na Wengine hawana haki

Ni kujisahu Katika maisha kuwa tulipelekwa shule ili kuisaidia jamii na si kuishi juu ya jamii

Nafsi yangu imenisuta sana na nimejiuliza mwisho ya Haya ni nini?

Hakika mwezi huu kuna kitu nimejifunza unapoondoka watu wanakuongelea vipi
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,757
2,000
Wanabodi, Kuomba msamaha sio ujinga bali ni kujitakasa mbele za Muumba

Napenda kutumia nafasi hii kuomba msamaha kwa wote niliowakosea kwa kujibu hovyo au kutukana Katika thread zangu, Reply Back na Comments zangu..
Hao unao waomba msamaha wanachofanya wenyewe ni propaganda (kumchafua kisawa sawa hayati, akumbukwe kwa mabaya badala ya wema).

Kwa kifupi umekubali kushindwa.
 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,355
2,000
Afadhali umeomba msamaha bila kushupaza shingo!! Usicheze na hasira ya Mungu watu wake wabapoonewa then ukachekelea na kuufurahia huo uovu au kuungana na muovu anapotenda uovu wake!

Maana unayoyanena wakati mwenzako anatendewa uovu hiyo laana itarudi kwako tu.

Sisi ni nani basi tusikusamehe, umesamehewa ila ajuae kama umeomba msamaha wa kweli ni yeye tu aonaye sirini!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom