NAOMBA MSAADA

Gervas Josiah

Member
Nov 4, 2021
6
20
Habari ya uzima
Nina taarifa fupi kuhusu kuhusu shule fulani ambayo maamuzi hufanywa kwa matakwa binafsi na sio ufuataji wa sheria. Wanafunzi wana adhibiwa kwa lengo la kutakwa kukubali kosa ambalo hawajafanya tena kwa vitisho vya kufukuzwa shule. Wanafunzi hupigwa fimbo mpaka maeneo yasio stahili. Kwa mfano, Kuna mwanafunzi wa Kidato cha pili ambaye alipigwa mpaka fimbo za kichwa. Kuna mwanafunzi alipigwa na mpaka kupelekea kupata donda mkononi na huku inampasa afanye mtihani wa Taifa.
Wengine huadhibiwa kwa mabomba tena Kiunoni au mgongoni. Lakini haya yote hufanywa na Mwalimu mwenye asili ya kiganda.
Mwalimu huyo amekuwa akijisikia kufukuza mwanafunzi leo ni sawa, kesho ni sawa pia maana hufanya for his interest. Wazazi wamelalamika sana kuhusu Mwalimu uyo ila kinachomsitili ni kuwa, ana urafiki wa Karibu sana na mmiliki wa shule jambo linalopelekea yeye kujikweza na kufanya yote bila hofu. Shule ni ya wavulana na wasichana ila akiwaona jinsia ME na KE wanasoma, yeye huwaita ofisini na kuwafungulia kesi ya Mapenzi. Wanafunzi hupigwa kwa hilo na wengine hushindwa kuvumilia na kuondoka makwao. Ni mwalimu ambaye anaweza kukupa pesa kwa mwanafunzi na asirudishe au amepewa na mzazi ila isimfikie mwanafunzi. Na pia, huwa treat wanafunzi kutokana na life status zao. Mtoto wa mwanajeshi akifukuzwa, mzazi akienda hupokelewa na mtoto kurudishwa ila wazazi wasio na wasifu kama huo huwatupilia mbali. Ana wakatia simu wazazi endapo watataka zungumzia maswala haya. Taarifa zilifikishwa kwa mwanasheria aliyewah fanya kazi ofisi ya makamu wa raisi ambaye kwa sasa ni Padri ila baada ya utambulisho, alikata simu.

Inauma sana maana hula jasho la mtu na hata wakija wakaguzi, yeye huwataka wanafunzi waiongelee mazuri shule na olewake atakaekeuka.
Mda mwingine hutoa adhabu kwa kosa lisiloendana na adhabu iyo. Yeye ni mwalimu wa nidhamu ila kaingia baada ya kumchafulia alietoka ili ashikilie nafasi yeye.
KINACHOUMA ZAIDI, kuna wanafunzi kadhaa wa kidato cha nne ambao wana mtihani wa taifa wiki ya pili mbele. Ni mwezi sasa tangu amsimamishe na masomo ila kosa lilikuwa ni la utawala na sio mwanafunzi. Unakuta mwanafunzi alipata 1.7 form 2 ila anapata 3 form four kisa maamuzi ya mwalimu huyo
Ombilangu: Awajibishwe na mwanafunzi arejeshwe kwasababu amefukuzwa kwa kosa la kutokutii walimu ila ilikuwa ni baada ya kusingiziwa so as he was trying to explain, wakasema anadharau. Inauma sana na anatabia ya kusimanga wazazi
Tafadhari, mwanafunzi huyo ni kiwango cha division one na ndo ufaulu wake tangu mwaka unaanza. Ombi langu arejeshwe na mwalimu apewe onyo

SHULE: GIFT SKILLFUL SECONDARY SCHOOL
LOCATION: MWENDAPOLE-KIBAHA
JINA LA MWALIMU HUSIKA: PIUS OWEN
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom