Naomba msaada

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,713
1,263
Wana JF salaam.

Mimi ni mjasiriamali, nimebobea kwenye ushonaji wa nguo aina zote. Nataka kuongeza masoko yangu, mwenye infuluence kwenye Tenda za ushonaji uniforms za shule, Hospitali, Hotel na nyinginezo naomba anipe contact za watu wenye interest nikaongeze masoko. Samples kwa anayetaka zipo.

Nitashukuru sana kwa msaada wenu.

Contact zangu ni 0787/0757 212122.

CD
 
Hongera kwa kuwa mjasiriamali CD
Naomba kujua kama kuna mahali unauza nguo zako hata kwa wanunuzi wa nguo moja moja ili tuweze kukuunga mkono!
Kila la kheri.
 
July nimehangaika kupata fundi although likuwa mkoani, unatafuta masoko ya nyanda za Kaskazini pia? If so, will make sure to have you bid next time around. Asante.

MamaEE asante sana kwa ushirikiano. Kote nafanya kazi as far as iko ndani ya uwezo wangu. namba zangu ni hizo anytime let me know.
Ubarikiwe sana mpendwa.

Carol
 
Hongera kwa kuwa mjasiriamali CD
Naomba kujua kama kuna mahali unauza nguo zako hata kwa wanunuzi wa nguo moja moja ili tuweze kukuunga mkono!
Kila la kheri.

Niko makumbusho, Mtaa wa Mali. Ukija nakupima nakutolea kitu cha size yako. Nashona express within 24hrs, nguo tayari. Karibu sana. Namba zangu zinapatikana muda wote. Karibuni sana.

CD
 
hizi ndizo topics ambazo zinaweza kuleta manufaa na possitive result katika jukwaa hili, nategemea kuwa thread hii itakuwa na changamoto nyingi sana kuboresha na kuwezesha biashara ya mtoa mada kufanikiwa zaidi, pia thread hii itatoa mwanga kwa wajasiriamali wengine wanohitaji mbinu mbali mbali za masoko na ubora wa bidhaa

CD je bidhaa zako zinakuwa na labels yenye kuonyesha type of fabric material, ironing suggestion, size na kadhalika, pia kwenye label weka contacts itakusaidia kama direct sales strategy

yangu ni hayo tu
 
Kama target markets zako ni shule, hospital, hotel na zingine kama hizo fanya utafiti kidogo. Nadhani hii haitakuwa kazi kubwa. Tengeneza business cards na vipeperushi halafu tembelea zile taasisi ambazo utagundua kuwa zina potential ya kuwa wateja wako.

Ongea na maofisa wao wa ununuzi au huduma za kitaasisi. Waachie mawasiliano yako na wewe chukua ya kwao ili uwe unawapigia simu kujua kama wana mahitaji yoyote. Vile vile unaweza kwenda na sampuli ya bidhaa yako ambayo inaweza kuwa kielelzo cha umahiri wako. Taasisi za umma zinatangaza tenda za wazi.

Sajiri kampuni yako ili uweze kukidhi vigezo vya kuwa mzabuni halafu jitose katika kushindania tenda. Kwa hili unapaswa kujielimisha kuhusu matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 (The Public Procurement Act, 2004) na Kanuni za Manunuzi za mwaka 2005 (Public Procurement Regulations, 2005). Kama unataka maelezo zaidi nitafute.
 
Wana JF salaam.

Mimi ni mjasiriamali, nimebobea kwenye ushonaji wa nguo aina zote. Nataka kuongeza masoko yangu, mwenye infuluence kwenye Tenda za ushonaji uniforms za shule, Hospitali, Hotel na nyinginezo naomba anipe contact za watu wenye interest nikaongeze masoko. Samples kwa anayetaka zipo.

Nitashukuru sana kwa msaada wenu.

Contact zangu ni 0787/0757 212122.

CD
Hongera bosi wangu... kaza msuli... dunia ishavaa bukta!!
 
CD. hongera sana.umechukua hatua nzuri kuanzia na familia yako ya JF. itakuwa Bomba zaidi ukiwa na online presence anza na Blogsite.hiyo tenda nipe mimi kwa makubaliano nafuu kabisa.

MkeshaHoi :Dunia imevaa bukta,hilo siyo tatizo kwani dada CD ataishonea Dunia Kanzu very Sooon. :)
 
Back
Top Bottom