Naomba msaada wa tatizo la mtoto kuvimba uume anapokojoa

jescalio

Member
Apr 19, 2015
7
3
Nina mtoto wa kiume wa miaka 2 sasa kuanzia asubuhi nimeshangaa kumuona akiwa anakojoa uume kule mbele kunavimba kama puto na mkojo unaenda pembeni hauendi mbele, nimempeleka hospital wanasema ni kwasababu ya infection (ana U.T.I) wakanishuri nimfanyie circumcision haraka.

Sasa naomba kujua undani wa tatizo hili na je ni infection tu au kuna tatizo jingine?

Asanteni
 
Huyo mtoto hana tatizo, na hilo govi ndio linasababisha mkojo kuenda pembeni. Kimsingi hakuna mahusiano kati ya bacteria infections na mkojo kwenda prmbeni.

Hapo yawezekana govi limenata kwenye utoko na mkojo unapokuja hadi kile kiongozi kinyenyuke na kujinasua kwenye utoko ndipo mkojo unakua umesha toka kwenye kitobo na kwa pressure mkojo unasukuma ngozi(govi) ili upate pa kupitia.
 
Yaani ajabu kweli madaktari walioona hawaaamimi, vipi utuamini sisi tusiomuona huyo kijana?
ndio nashangaa, ameshaambiwa solution anasubiri nini angefanya akaona vitaleta matokeo gan kama ugonjwa utatokomea au hautaondoka ajabu kakimbilia jf mtoto anaumia
 
Nina mtoto wa kiume wa miaka 2 sasa kuanzia asubuhi nimeshangaa kumuona akiwa anakojoa uume kule mbele kunavimba kama puto na mkojo unaenda pembeni hauendi mbele, nimempeleka hospital wanasema ni kwasababu ya infection (ana U.T.I) wakanishuri nimfanyie circumcision haraka. Sasa naomba kujua undani wa tatizo hili na je ni infection tu au kuna tatizo jingine? Asanteni
kamtahiri araka
 
Katimize agano la ibrahimu kwanza kisha uje utupe mrejesho.
Ukitafuta majibu nje ya yale ambayo umeshapewa utachelewa kupata matokeo chanya
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom