Naomba msaada wa tatizo la kusikia joto na mdomo kuwa mchungu

Tyalambu

Member
Jul 9, 2017
18
4
Habari wadau?

Nina tatizo la mwili wangu kuwa na joto muda wote na mate yanakuwa ya uchungu na hilo joto inafikia kipindi mpaka mwili unaniwaka sana moto!

Nilipima kipimo cha full blood picture nikaambiwa niko fresh! ila nikamuambia Doctor unaniambia niko fresh ila najisikia joto ambalo siyo la kawaida katika mwili wa binadamu mwenye afya timu?

Akasema subiri nikupime joto alivyonipima akanambia kuwa joto lako lipo katika kiwango ambacho ni Standard cha binadamu mwenye afya njema! nikamwambia basi kama ndiyo hivyo kuanzia leo siendi hospitali tena kuhusu hili tatizo haiwezekani joto nalolihisi katika mwili wangu ni kali sana alafu wewe unasema joto liko Standard. Tangu siku hiyo sikuhangaika tena ila mpaka leo bado naishi na hilo tatizo.

NOTE: Tatizo hili halinizuii kufanya jambo lolote kuanzia kula chakula cha aina yoyote, kunywa kinywaji cha aina yoyote (ila pombe situmii) wala sijawahi kupoteza hamu ya kula japokuwa muda wote mdomo ni wa uchungu! na kazi zangu zinaendelea kama kawaida kwa kifupi huwezi jua kama natatizo mpaka nikuambie!

NOTE: Nishatembea kwa waganga wa kienyeji kama wa3 hivi baada ya kutoka hospitali lakini pia wameshindwa kutibu tatizo nishatumia dawa nyingi za kienyeji tena chungu kupita maelezo lakn wote wamefeli!

Asanteni sana Nategemea ushauri mzuri kutoka kwenu!
 
Kiukweli madaktari wanatupoteza sana,yaani madaktari wa tz wao ni kubahatisha bahatisha tuu mambo.mimi nina tatizo ambalo kila daktari ananipa dawa anayoijua
 
Huyu jamaa anatakiwa sasa, aanze kula vizuri, ampumzishe mwili wake, afanye mazoezi na amrudie Mungu wake
 
Back
Top Bottom