Naomba msaada wa Muongozo wa kuanzisha kikundi cha kuinuana kiuchumi/Saccos | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa Muongozo wa kuanzisha kikundi cha kuinuana kiuchumi/Saccos

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Chigwiyemisi, Mar 12, 2012.

 1. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wadau nawasalimu.Mimi na wenzangu tumeamua kuanzisha kikundi ambacho kitakuwa na malengo ya kujiendeleza na kubadilishana mawazo na utaalamu. Ni kama SACCOS lakini tunategemea kuwa na malengo mtambuka. Naomba yeyote mwenye SAMPLE ya katiba au document yoyote ambayo itatupatia muongozo wa kuanzisha kikundi chetu au SAMPLE ya katiba ya kikundi kama tunachotegemea kuanzisha aniwekee hapa jamvini itusaidie!Natanguliza shukurani.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hongera kwa kutaka kujikwamua na umasikini

  - Ila naomba uelewe vifuatavyo
  1. Kikundi na SACCOS ni vitu viwil tofauti kabisa

  2. Uanzishwaji wa SCOS ina idadi ya members na kikundi kina idadi ya members

  3. Na SACCOS mara nyingi inadili na kuweka na kukopa na sijajua kama ndo lengo lenu la kuweka na kukopa

  4. Kikundi ndo kinaweza fanya mambo mengi hata likiwemo la kuweka na kukopa

  5. Mkianzisha kikundi kuna furusa za kibiashara mnaweza kuzikosa kwa sababu kikundi kufanya biashara na makampuni inakuwa ngumu kidogo na mtakuwa mnabanwa na sheria za vikundi na mambo ya TRA

  6. kama mko siriaisi na kama mmeisha jipanga na tiyali mna mawzo yenu ya biashara mnaweza tu fungua kampuni ya mtaji mdogo na hata mkienda TRA kitengo cha Elimu kwa walipa kodi watawapa elimu ya Ulipaji kodi ya makampuni mtaona kwamba ni rahisi sana kuliko kuogopa kampuni kisa TRA,

  7. Kwa dunia tuliyopo sasa kampuni inaply sehemu kubwa sana katika kufanya biashara yoyote ile na si kwamba kampuni kuindesha ni mpaka muwe na mtaji wa mamilioni, no kuna kapnu zinasajiriwa kisheria na zinamitaji ya elfu 80, tu
   
 3. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Chasha nashukuru sana kwa maelezo na ushauri wako. Kwa hakika umenipa ufafanuzi mzuri sana pamoja na kwamba ni kwa ufupi lakini nimepata mwanga. Naamini kuwa una uelewa mpana sana wa masuala haya, kama inawezekana naomba tuwasiliane nje ya jamvi ili uwe msaada kwangu na kwa wenzangu!
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  poa mkuu usijari tuko pamoja
   
 5. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  napenda kukushauri biashara ni wazo ulilonalo hayo mnayowaza ndo yawekeni kwenye maandishi kwani ndo malengo yenu ukipewa sample ya katiba utakuwa unatumia mawazo ya wengine huenda ukasumbuka kufikia lengo.
  na kama itabidi kutumia katiba ya vikundi vingine iwe kuboresha mlichokwisha andaa.
  MY TAKE.

  HONGERA KWA KUTHUBUTU UNAWEZA NA UTAFANIKIWA WEKA BIDII MBELE.
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, katiba sio objectives pekee, kwa hiyo wanaweza wakatofautiana kwenye objectives na bado mfumo wa uandishi wa katiba ukaendana.
  You don't need to reinvent the wheels katika mazingira haya
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mtafute mwenyekiti wa JE Saccos , hii ni saccos iliyoanzishwa kwa kupitia platform ya JF

  yupo humu kwa Id ya "The Finest" atakusaidia
   
Loading...