Naomba msaada wa mawazo,nifanye nini ili niweze kuhama?

fikirijohnas

Member
Nov 10, 2018
46
25
Mimi ni mwajiriwa serikalini,kipindi TAMISEMI hawajasitisha uhamisho,nilipata mtu wa kubadilishana naye kituo cha kazi yeye ahamie katika halmashauri yangu nami niende halmashaurini kwake.Nilipitishiwa barua yangu ya kuomba uhamisho na mkuu wangu wa kituo lakini ilipofika halmashauri nikaambiwa kuwa ombi la uhamisho wangu limekataliwa kutokana na upungufu wa watumishi,hivyo nikaambiwa nisubiri ajira mpya au nitafute mtumishi wa kubadilishana naye.
Niliamua kuandika barua nyingine kwenda kwa katibu tawala wa mkoa kupitia kwa mkuu wangu wa kituo,na mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni mwajiri wangu.Ajabu ni kwamba,hadi sasa sijapitishiwa barua yangu,bado iko halmashauri japo niliipeleka tangu mwaka jana mwezi December.Kila nikienda kufuatilia naambiwa nisubiri nitajibiwa,mara faili langu limepotea na sababu zingine za aina hiyo.Mara ya mwisho nilipoenda nilikuta faili limerudishwa masjala ilhali barua yangu haijapitishwa wala sijaandikiwa barua yoyote kujibiwa.Naomba msaada wa mawazo,nifanye nini ili niweze kuhama? Nina sababu za msingi zinazonifanya niombe uhamisho.Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom