Naomba msaada wa mawazo namna ya kutatua hii changamoto

Stretcher

Member
Oct 24, 2020
34
24
Habarini, Mimi niliajiriwa mwaka 2005 mwalimu wa sekondari kwa tiketi ya leseni, nilitimiza miaka 2 ndipo nikaenda masomoni.

Nilienda kusoma degree ya ugavi tofauti na ruhusa baadae. Nilihitimu 2010 sikurudi kazini hali iliyopelekea Mimi kuwa mtoro.

Niliamua kushugulikiaa suala la kurudi. Kazini mwaka 2018 mpaka sasa nimepata msamaha kwa katibu mkuu. Shida ni tangazo la waalimu kuondolewa kwenye payroll la mwàka 2017.

Je, mnanishauri nifanyeje nini kwani. Barua ya kurejeshwa kwenye payroll. Ninayo ishu ni utumishi tu.
 
'Tangazo la waalimu kuondolewa kwenye payroll mwaka 2017' litolee ufafanuzi mzuri hili ili lieleweke.
 
'Tangazo la waalimu kuondolewa kwenye payroll mwaka 2017' litolee ufafanuzi mzuri hili ili lieleweke.
Ni tangazo ambalo lilitoka September 2017 likiwa na heading TANGAZO
KUWAONDOA WALIMU TARAJALI(TEACHER TRAINEES)KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MSHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA MWEZI SEPTEMBA 2017 tangazo hili nilipewa na afisa utumishi akisema hilo ndio linalomzuia kunirudisha kwenye mfumo; tangazo lenyewe ni hili
tmp-cam-1186924776.jpg
 
Duuuh pole... Hapo tafuta TU kazi nyingine
Ahsante, pamoja na hilo niendelee kusubiri maoni ya wadau wengine.

Maana ishu yangu ilianzia kwa katibu mkuu kiongozi kwa barua yenye maelezo marefu sana yakiambatana na nyaraka zote yaani barua na vyeti vyote.
 
Ww ulifukuzwa kazi sababu ya utoro kazi ni so huwezi kurudi kwa system wala kuajiriwa tens na serekali

Ulishidwa kuchanga karata zako vizuri

Kosa lako ni utoro kazini na sio kwenda kusoma
 
Sasa kama issue yako ilianzia kwa katibu mkuu kiongozi na akaandika barua ndefu na maelezo kibao si AKURUDISHE kazini...kwa nn unakuja kuomba mawazo yetu?

Tukikwambia umeondoka kwa utoro na kosa sio kusoma una-mind..!

Tukikwambia tafuta kazi nyingine una-mind

Unataka ushauri wa kukutia moyo au??

Maana katibu mkuu kiongozi angeandika tu order ya kukurudisha kazini....

Unasumbua tu Great thinkers hapa.
 
Habarini, Mimi niliajiriwa mwaka 2005 mwalimu wa sekondari kwa tiketi ya leseni, nilitimiza miaka 2 ndipo nikaenda masomoni.

Nilienda kusoma degree ya ugavi tofauti na ruhusa baadae. Nilihitimu 2010 sikurudi kazini hali iliyopelekea Mimi kuwa mtoro.

Niliamua kushugulikiaa suala la kurudi. Kazini mwaka 2018 mpaka sasa nimepata msamaha kwa katibu mkuu. Shida ni tangazo la waalimu kuondolewa kwenye payroll la mwàka 2017.

Je, mnanishauri nifanyeje nini kwani. Barua ya kurejeshwa kwenye payroll. Ninayo ishu ni utumishi tu.
Kweli Maisha mzunguko, Dunia duara. Yaani kutoka Unaibu Rais, Bunge la Africa mapaka kupigania ajira ya ualimu? Pole Sana Mkuu
 
Ww ulifukuzwa kazi sababu ya utoro kazi ni so huwezi kurudi kwa system wala kuajiriwa tens na serekali

Ulishidwa kuchanga karata zako vizuri

Kosa lako ni utoro kazini na sio kwenda kusoma
Hapana, ni hivi mimi sikufukuzwa kazini kwa sababu ya utoro au sababu yoyote. Niliondolewa kwenye mfumo wa payroll kwa sababu ya kutokuwepo kazini baada ya kuhitimu chuo kwa ruhusa niliyopewa, waliniondoa na hawakunipa barua ya kuniondoa kwenye mfumo hata barua ya kunifukuza kazi sina; kwa hiyo kuwa mtoro ni baada ya kuondolewa kwenye mfumo wa mshahara mpaka nilipoanza kushughulikia kurejeshwa kwenye payroll.

Suala ambalo kama nilivyosema lilihitimishwa shauri na katibu mkuu, wizara ya elimu...Sasa shauri la utoro limeshahitimishwa ndio kiwe kigezo cha kutonipokea halimashaurini? Hapana maana msamaha nimeshaupata tens toka Ikulu mpaka wizarani. Ishu kubwa pale halmashaurini wameshindwa kutokana na tangazo.

Kweli sikuchanga karata vizuri kwa sababu sikufahamu yatanikuta haya lakini ushindi upon kwa sasa cha muhimu suala lilipofikia kwani uwezekano wa kunirudisha kazini upon tofauti na kuniajiri tena serikalini haiwezekani kwa sababu natambulika kwenye mfumo nilishaajiriwa serikalini. Cha msingi ni tangazo na kurejeshwa kwangu kwenye system.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom