Naomba msaada wa mawazo maana nimeshindwa kujua nini cha kufanya

Evance2006

Member
Dec 27, 2016
60
27
Wadau mimi ni kijana mwenye miaka 27 nimemaliza chuo mwaka 2015.. Kuna binti nipo nae katika mahusiano kwa kipindi kirefu na kwa bahati nzuri tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume ambae kwa sasa ana umri wa mwaka mmoja na nusu.

Kwa sasa huyo mchumba wangu niliyezaa nae yupo chuo mwaka wa tatu, na tunawasiliana vizuri sana na kibaya zaidi kwao wananitambua japo ni kwa simu.
Hivi majuzi kama mwezi wa 10 nilimpata binti mmoja tukawa naye katika mahusiano kiukweli binti ananielewa sana na ananipenda sana...

Kibaya zaidi hana anachotaka juu yangu zaidi ya mapenzi!!! Ananisaidia vitu vingi sanaa... Na anadiriki kuamini kuwa mimi nitakuwa mume wake... Kiukweli sijawahi kumwambia kuwa nina mtu ambaye tayari nimezaa nae... Na ukweli ni kuwa na mimi nampenda kwa nafasi yake!! Wakati huo huo kuna mtu ambaye anajua mimi ni mme wake(mama mtoto wangu)....

Sasa shida inakuja nifanye nini ili niweze kumuacha huyu binti ambaye ni mpenzi wangu mpya.... Maana lengo langu ni kuishi na mama mtoto wangu... Ninavyoona nikiendelea kukaa na huyu binti bila kumwambia ukweli nikija kumwacha au kumwambia baadae nadhani nitamuumiza pakubwa!!!!

Lengo langu nimuache mapema maana mke wangu anamaliza chuo mwaka hui hivyo uwezekano wa kuishi nae ni mkubwa muda sio mrefu..
USHAURI WENU WADAU MWENZENU NIMEWAZA NIMEKOSWA MAJIBU
 
Umezaa na mtu ....... Na anatambua kuwa wewe ni kama mmewe mtarajiwa...kwa sasa mchumba wako yupo chuo mwaka wa Tatu semester ya kwanza......wakati huo huo wewe unafanya ukahaba wa kuparamia mwanamke mwingine......Tabia gani hizi?....kwa hiyo unataka ushauri wa kupotoshwa......wakati huo eti na wewe ni Mwalimu ..... Maombi ya nafasi za kazi
Job application......acha wanafunzi waendelee Ku fail...
Tabia yako hata shetani hana.
 
Ww unampenda yupi?!...acheni kuwaumiza watt wa watu kwa ahadi za uongo mnawapotezea muda mwingi labda kuna mtu alitaka kumuoa lkn akamkataa akitegemea ww una malengo nae


Bora umkaze ukimbie kuliko kujifanya unataka kuoa.
 
Kwani alikutongoza au ulimtongoza?wakati unamtongoza haukujua kama una mtarajiwa wako?sasa unataka ushauri wa nini?mbona hauna uruma wewe?
 
Kwani alikutongoza au ulimtongoza?wakati unamtongoza haukujua kama una mtarajiwa wako?sasa unataka ushauri wa nini?mbona hauna uruma wewe?
Sio tu hana huruma,hana akili zs kutosha pia. Graduate mzimw unaleta mambo ya kitoto hapa. Hili jambo lilitakiws liletwe na huyo kahaba mwenzako unayemdanganya hujazaa. Halafu eti tunategemea kupata wasomi wakaendeshe viwanda. Kwa post yako hii watakaokushauri positively kwa huyo kahaba mwenzako nadhani anatakiwa apimwe ubongo. Nyinyi ndiyo mnajaza watoto wa mitaani.
 
Hatuwezi kuwavumilia mkuu. Ukisema uwavumilie kuba siku wataomba ushauri namna(style) ya kugegeda. Halafu hapo anatamba mtaani koote ooooh ! Mimi graduate, graduate gani anafanya mambo haya
Mkuu unajua hawa watoto nidhamu yao imeisha na wanajua kila kitu ni chakujadili hadharani bila kujua mengne huwa tunayamaliza nyumbani kwetu hatupeleki hadharani
 
Wewe ni muaji kabisa na huna huruma kabisa kazi yako kujirusha hufikiri hata mtoto ; dada wa watu amekubali umezaa naye halafu unaturetea stori za kijiga nataka nikuambia hakuna binti nyakati hizi asiyetaka kuolewa hawa watu wanafanya kila jitihada kuwapata wanaume rudi kwa mlie zaa naye acha kurukaruka
 
Nyie ndo mnajaza single mothers mitaani. Jiongeze mwenyewe... Mxiuuuu. Umzalishe kisha umuache. Nyie ndo wale midume suruali. Kisa unasaidiwa na huyo mwingine unataka kumwacha mzazi mwenzio
 
Back
Top Bottom