Naomba msaada wa mawazo kuhusu mkopo kutoka Bayport

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Wana uchumi wenye uzoefu naomba ushauri nina deni Bayport wa sh milioni 9.9 lililotokana na mkopo wa sh, milioni 5.2 kiukweli riba zao ni kali,,,, nimekopa kwa miezi 36,,,,,,, bado miezi 3 niwe na miezi 24,, nimewaza kwenda kupunguza ikiwezekana kufuta deni kabisa,,, muhudumu kaniambia Sina haja ya kuandaa hela pindi niendapo tutaandikishana tu mkataba na pia kasema huo mkataba hatutajali riba wataangalia nimefikisha kiasi changu cha deni na kumaxmize makato ili nimalize mapema je ni sawa??? Na kwa hesabu zangu miezi hiyo 24 ntakuwa nimelipa milioni 6 kama riba hawataangalia inamaana deni Sina inamaana wataniandikisha mkataba wa kufuta deni????? Msaada pls kwa uzoefu wenu
 
mkiweza kuandikishiana hiyo miezi mitatu itapotea na riba ya milioni 6 itakuwa ya miezi itakayobaki. kuwa makini
 
Unapohitaji ushauri ni vizuri ukajitahidi kutumia lugha "lahisi" ili uweze kueleweka. Jiepushe kuchanganya lugha.

Mie sijakuelewa kabisa. Hivi ulipoenda wamekuambia huna haja ya kulipa kiasi kilichobaki au unakilipa kwa kutoa kiasi fulani huku mkiandikishana mkataba wa kufuta deni?
 
kwakweli mkuu uandishi mwingine huwa ni sheedah. Mtu mzima anaandika utadhani anaendesha baiskeli.

Inamlazimu msomaji atumie nguvu nyingi kumuelewa. kazi kweli kweli...
 
Walisema haina haja ya mimi kupeleka fedha Bali wao wataniandikisha mkataba mwingine kwa kuangalia deni tu nimelipa kiasi gani pasipo riba ndipo napata mkanganyiko kwasababu ndani ya miezi 24 deni pasipo riba litakuwa limeisha je uhalisia kiuzoefu iko vp hii??
 
kwakweli mkuu uandishi mwingine huwa ni sheedah. Mtu mzima anaandika utadhani anaendesha baiskeli.

Inamlazimu msomaji atumie nguvu nyingi kumuelewa. kazi kweli kweli...
Hahaha #kaveli unapokosoa toa kasoro,,, kwamfano mjumbe aliyetangulia kasema kuchanganya lugha si vyema,,, kwahivo pole mtu mzima pia kutoa kasoro yenye kasoro ni shida,,, LOL
 
Walisema haina haja ya mimi kupeleka fedha Bali wao wataniandikisha mkataba mwingine kwa kuangalia deni tu nimelipa kiasi gani pasipo riba ndipo napata mkanganyiko kwasababu ndani ya miezi 24 deni pasipo riba litakuwa limeisha je uhalisia kiuzoefu iko vp hii??

Huenda ni kweli maana hao jamaa RIBA zao si tu zipo juu bali ni "wizi wa mchana". Kwa kiasi ulicholipa hata wakikuambia imetosha tayari wameshapata "faida ya kupindukia".

Ni vizuri kuwa makini wakati unapotaka kukopa kwani taasisi nyingine za fedha zinataka" Super normal Profit ".
 
nakushauri uwe makini unapotaka kumaliza deni hili, ikibidi tafuta mwanasheria akusaidie hili kisheria, pia nakushauri ukimaliza huu mkopo upumzike kwanza bila kukopa.
 
Wana uchumi wenye uzoefu naomba ushauri nina deni Bayport wa sh milioni 9.9 lililotokana na mkopo wa sh, milioni 5.2 kiukweli riba zao ni kali,,,, nimekopa kwa miezi 36,,,,,,, bado miezi 3 niwe na miezi 24,, nimewaza kwenda kupunguza ikiwezekana kufuta deni kabisa,,, muhudumu kaniambia Sina haja ya kuandaa hela pindi niendapo tutaandikishana tu mkataba na pia kasema huo mkataba hatutajali riba wataangalia nimefikisha kiasi changu cha deni na kumaxmize makato ili nimalize mapema je ni sawa??? Na kwa hesabu zangu miezi hiyo 24 ntakuwa nimelipa milioni 6 kama riba hawataangalia inamaana deni Sina inamaana wataniandikisha mkataba wa kufuta deni????? Msaada pls kwa uzoefu wenu

Jambo kama hili kaka inategemea na mkataba mlioandikiana ama mtakaoandikiana! Ila tu kwa kukupa mfano kama tumekuelewa vizuri itakuwa ni hivi!!
inategemea mkopo na mkopo! ama kampuni na kampuni but a basic principle ni kama ifuatavyo:-
kama umekopesha M5 na kuwekeana muda wa miezi 36 = miaka miaka mitatu! hapo huwa na riba inaweza kuwa calculated kuonyesha mpaka miaka mitatu ikiisha utakuwa umelipa kiasi gani.
sasa chukulia mfano huu rahisi ya kwamba labda riba yako kwa mwaka ni asilimia 20%. na mwakani pia hivyo hivyo kwa kile kiwango kilichobaki. na mwaka wa tatu pia mlolongo ni huo huo.
wewe baada ya miaka miwili ukajikuta umezoa kitita sehemu na kutaka kumalizia deni lako ili uachane nao. na mpaka sasa miaka miwili ukihesabu unakuta ushawapa M6 , hii ni zaidi ya kile kiwango ulichokopesha lakini sio pesa yote ni deni lako! M6 sita hii utakuta ni m3.5 ya deni na hizo mbili na nusu ni riba waliokuwa wanakuchaji katika miezi ya miaka hiyo miwili iliyopita. sasa leo kama umeamua kumaliza deni na wanakwambia kwamba kama ni hivyo hutolipa riba. Maana yake ni hivi:-

wanatazama kiwango ulicholipa mpaka sasa. ni hizo M6. wanatoa riba charges zilizokuwepo katika kipindi hicho kilichopita ili kujua ni ngapi katika deni lako umeshalipa ukiondoa charges za riba na kama kuna mengine. Sasa kwa sababu mwaka huu hutolipa kila mwezi na umeamua ulipe leo zote zillizo baki! maanake kama hapo juu ukitoa riba za zamani unakuwa umelipa M3.5 katika M5 ulizokopeshwa. kwa hiyo leo unaenda na 1.5M kumalizia deni lako bila kulipia riba ya hizi pesa zilizobaki kwasababu umezileta kwa mkupuo mmoja. Hii maanake hulipi riba kwa deni lililobaki. lakini sehemu ya deni ambayo umekua ukilipa kwa miezi iliyopita riba inakuwa ushalipa na hiyo haihesabiki kama ni sehemu ya deni. bali ni riba. kwa hiyo kama ulikopesha M5 na leo ushalipa 6 na umebaki na miezi kadhaa. itahesabiwa iyo miezi na unailipa yote kwa pamoja bila riba. hiyo ndio maanake.
Tahadhari:- Hii ni general principle, sasa inategemea na mkataba ulioandikisha wamekubana vipi. ila kama washakwambia utamaliza deni bila riba maanake ndio hiyo juu. sio kwamba ukihesabu unakuta deni ushamaliza! la hasha deni hujamaliza Deni lako liligawanywa kwa miaka hiyo mitatu na juu yake pakawa na riba katika kila mwezi. ndio maana leo zipo M6 . ila kutoka hapa utalipa deni lilibaki na wataondoa riba ambazo ulitakiwa kulipa juu ya deni kila mwezi.
nadhani umepata kidogo ingawaje nimezunguka sana. na kama nimekosea mafundi watasahihisha hapa.
kila la kheri.
 
Thanks kitope kwa kushare idea nami nashkuru kiasi nimepata mwanga
 
Unapohitaji ushauri ni vizuri ukajitahidi kutumia lugha "lahisi" ili uweze kueleweka. Jiepushe kuchanganya lugha.

Mie sijakuelewa kabisa. Hivi ulipoenda wamekuambia huna haja ya kulipa kiasi kilichobaki au unakilipa kwa kutoa kiasi fulani huku mkiandikishana mkataba wa kufuta deni?
Rahisi sio Lahisi mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom