Naomba msaada wa kwenda kusomea uchungaji

Jacobunge

Senior Member
Oct 10, 2013
129
15
Bwana asifiwe,,
Mimi ni muumini wa kanisa la wadvetista msabato
katika maisha yangu nilikuwa na ndoto ya kwenda kusomea uchungaji tangu nikiwa shule ya msingi
lkni nilipomaliza kidato cha nne nilitafuta nafasi nikaambiwa hawachukui kidato cha nne,,au labda nikafanye mtihani unaoitwa mature entry(kama nimekosea mnirekebishe) lkn masharti ya mtihani ule ni kuwa na umri usiopungua miaka 22
baada ya kuonekana nimekosa vigezo hivyo niliamua kwenda kusomea ualimu wa shule ya msingi(mpaka ss mimi ni mwalimu)

lakini bado nina nia ya kwenda kusomea uchungaji lkni cjui nifanyaje ili nifanikishe ndoto yangu

NB;mimi niko tyr kuacha utumishi wa serikali kama nitaona kuna mlango wa kwenda kufanikiwa ndoto yangu
 
wachungaji wenyewe siku hizi mnaenda kusomea kutupiga tu na isitoshe kwa ubinafsi wa wasabato inabidi ukaombe msaada kwa wasabato wenzako, arusha tengeru wana university mpaka waislamu wanasoma ni kwa nini wasikupe sponsorship wewe ili uje kulitumikia kanisa lao?
 
una mawazo mazuri,,nitachambua pumba nitatoa na mchele ntachukua
 
Mbona ni rahisi sana kwa kuwa umeajiriwa tumia mwaka mmoja tu kusoma upate cheti cha form six kuna hiyo program ukifaulu tumia hicho cheti kuomba hiyo nafasi
 
nipe namna ya kufanya ilihali nipo kwenye utumishi
 
Program hii inaendeshwa na waalimu wa part time sana sana muda wa mchana moaka jioni ila sijui mchakato wa kujiandikisha waulize waliosoma 5&6 kwa. Njia hii mkuu tena wanafaulu vizuri sana
 
mkuu chuo cha wasabato cha arusha kipo chini ya tcu ndio maana kuna vigezo vingi
ila nakushauri uende bugema university uganda wanachukua form four kufanya degree ya theology pia ada yao ninafuu sana
 
wazo zuri,uchungaji chuo kipo arusha university tembelea website yao kuna maelekezo yote.
 
Bwana asifiwe,,
Mimi ni muumini wa kanisa la wadvetista msabato
katika maisha yangu nilikuwa na ndoto ya kwenda kusomea uchungaji tangu nikiwa shule ya msingi
lkni nilipomaliza kidato cha nne nilitafuta nafasi nikaambiwa hawachukui kidato cha nne,,au labda nikafanye mtihani unaoitwa mature entry(kama nimekosea mnirekebishe) lkn masharti ya mtihani ule ni kuwa na umri usiopungua miaka 22
baada ya kuonekana nimekosa vigezo hivyo niliamua kwenda kusomea ualimu wa shule ya msingi(mpaka ss mimi ni mwalimu)

lakini bado nina nia ya kwenda kusomea uchungaji lkni cjui nifanyaje ili nifanikishe ndoto yangu

NB;mimi niko tyr kuacha utumishi wa serikali kama nitaona kuna mlango wa kwenda kufanikiwa ndoto yangu

Mkuu nakuombea ufanikiwe alafu ukishaingia huko ukapige marufuku wanawake kuwa wachungaji.
 
Unapopokea Nguvu ya Roho Mtakatifu huambatana na karama mbalimbali kama uponyaji, kuhutubu(uchungaji) nk, hivyo Roho wa Mungu hukuongoza unachopaswa kufanya. Ukifanya kitu kwa kujisikia bila kuongozwa na Roho wa Mungu tarajia huduma yako kuanguka baada ya ya muda mfupi
 
Back
Top Bottom