Naomba msaada wa kutatua tatizo la kuumwa mafua wakati kulala na kupiga chafwa asubuhi wakati wa kuamka

kibori nangai

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
1,066
1,315
Habari wana jamvi,

Naposti kwa niaba ya jamaa yangu.

Amekuwa anasumbuliwa na mafua toka mwaka 2006. Asubuhi akiamka anapiga chafya sana, na mara nyingi akitembelea maeneo ya baridi ndio hali inazidi kuwa mbaya sana.

Anaweza kuumwa mafua hadi anapotoka maeneo hayo.

Amepima mara nyingi akambiwa ana aleji ya na baridi na mambo mengi ambayo katika maisha ya kawaida huwezi kuepuka.

Mdau anaomba msaada afanye nini aweze kuondokana na hii hali. Yupo tayari kwa ushauri wowote, msaada wowote kwa gharama yoyote.

Amekuwa muhudhuriaji wa maduka ya dawa kununua madawa yote aleji.

Msaada tafadhali nafahamu wapo watakaopinga lkn sitojali wale watakaoshuri vyema. Nitaufikisha kama watakavyowasilisha.

Ahsanteni sana.

Nitawashukuruni sana msaada utakaosaidia kukuona hii hali.
 
Habari wana jamvii
Naposti kwa niaba ya jamaa yanguu
Amekuwa anasumbuliwa na mafua toka mwaka 2006
Asubuhi akiamka anapiga chafwa sana na maranyingi akitembelea maeneo y baridi ndio hali inazidi kuwa mbaya sana...

Hiyo inaweza kuwa ni allergy lakini pia anaweza kwenda kumuona ENT Surgeon
 
Tafuna vitunguu swaumu na tangawizi kwa pamoja asubuhi na usiku ukisindikiza na maji ya moto yenye limao kama chai(ila sio chai) huku ukisubiri siku 14.

Ukisikia maisha mafupi ndio sasa.
 
tafuna vitunguu swaumu na tangawizi kwa pamoja asubuhi na usiku ukisindikiza na maji ya moto yenye limao kama chai(ila sio chai) huku ukisubiri siku 14.
Ukisikia maisha mafupi ndio sasa.
Sawaa mkuu wanguu ngoja nitamuambie afanyie kazi hiiii
 
Nikiwa mikoa ya baridi kipindi cha masika chafya za kutosha asubuhi. Nikiwa daslam,Tanga au Zenji hakuna chafya wala mafua mwaka mzima.
Huo ni mzio .
 
Daaa... aisee... Hata mimi nina shida hiyo nikilala usingini nilishtuka tu lazima nipige chafya za kutosha na nyumba nzima watajua jamaa kaamka mbali na hapo huwa napiga chafya sana nikiskia harufu ya marashi spray na pafyumu awali nilikuwa nikisumbuliwa na tatizo la kutokwa damu puani kila nikipatwa na mafua ambapo nilipata tiba yake.
 
Hiyo ni allergy

Kuna kpindi nilikua Kama huyo jamaa akoilikua Kila nikiamka asubuhi najikuta nna mafua
Nikisogea sehem yyte yenye vumbi napata mafua.

Ila baada yakuanza kutafuna tangawizi Kila siku Hali hiyo ilipotea mpaka leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom