Naomba msaada wa kupata Waraka wa utumishi wa umma no 2, wa mwaka 2018, unaokataza malipo ya uhamisho

Iwe iliomba uhamisho au ulihamishwa kwa matakwa ya ofisi yako bado una haki ya kulipwa stahiki za mtu anayehama.
Labda tu pale mnapokubaliana katika terms ya uhamisho ulioomba kuwa utajigharamia wewe mwenyewe.
 
Hapana hakuomba kahamishwa na mwajiri, ngoja niombe hiyo barua nilete hapa maana nimestuka baada ya kuona hiyo barua nikadhani ndio utaratibu mpya umeanza maana nimetafuta huo waraka bila mafanikio ndio maana nikaja jukwani hapa kujua je upo au imetumika janja janja watu wapige mafungu
 
Akikubali kuhamishwa bila pesa basi atakuwa lofa. Labda ni uhamisho wa ndani ambao atahamia kwenye eneo karibu na kituo chake cha kazi cha awali
 
Hapana hakuomba kahamishwa na mwajiri, ngoja niombe hiyo barua nilete hapa maana nimestuka baada ya kuona hiyo barua nikadhani ndio utaratibu mpya umeanza maana nimetafuta huo waraka bila mafanikio ndio maana nikaja jukwani hapa kujua je upo au imetumika janja janja watu wapige mafungu
Hakuna kitu kama hicho. Kama hukuomba kuhama na ni mwajiri amekuhamisha ni haki yako kulipwa
 
Sheria ndio ipo hivyo ila uhalisia haupo hivyo. Waajiri ni untouchable wanafanya vile wanavyojisikia, wanalipa pale tu wanapoona inafaa kulipa na pia kwa watu wawatakao wao.
 
Mtumishi wa Umma anapopata uhamisho wa bila kujiombea au wa kujiombea kama amekaa kwa miaka 5 au zaidi katika kituo anachoomba kuhama anastahili kulipwa malipo ya uhamisho kama ifuatavyo:
Screen Shot 2021-05-25 at 11.00.33 AM.png

Malipo haya yanatakiwa kufanywa wakati wa uhamisho na sio kama madai. Yaani Mtumishi hapaswi kujisafirisha ili baadae ndio afanye madai ya fedha aliyotumia. Mwajiri anatakiwa kuhakikisha ametenga fedha ya kumhamisha mtumishi ndipo afanye uhamisho. Muda wa Malipo ya madai haya ni ndani ya siku 14 toka mtumishi aliporipoti kituo kipya, nje ya hapo inapaswa yawe ni makubaliano ya mwajiri na mwajiriwa, akuombe uvumilie.
 
Sheria ndio ipo hivyo ila uhalisia haupo hivyo. Waajiri ni untouchable wanafanya vile wanavyojisikia, wanalipa pale tu wanapoona inafaa kulipa na pia kwa watu wawatakao wao.
Sajo kwakua mwajiri ana boss wake je wakienda ngazi za juu uko haiwezi wasaidia wakapata stahiki zao
 
Wanaweza, waandike malalamiko Tume ya Utumishi wa Umma. Ila yatachukua zaidi ya mwaka kupata nafasi ya kusikilizwa
 
Mtumishi wa Umma anapopata uhamisho wa bila kujiombea au wa kujiombea kama amekaa kwa miaka 5 au zaidi katika kituo anachoomba kuhama anastahili kulipwa malipo ya uhamisho kama ifuatavyo:
View attachment 1797038

Malipo haya yanatakiwa kufanywa wakati wa uhamisho na sio kama madai. Yaani Mtumishi hapaswi kujisafirisha ili baadae ndio afanye madai ya fedha aliyotumia. Mwajiri anatakiwa kuhakikisha ametenga fedha ya kumhamisha mtumishi ndipo afanye uhamisho. Muda wa Malipo ya madai haya ni ndani ya siku 14 toka mtumishi aliporipoti kituo kipya, nje ya hapo inapaswa yawe ni makubaliano ya mwajiri na mwajiriwa, akuombe uvumilie.
Nadharia watu wa hovyo hawalipi hata miezi 4 unadai ... ujinga na unakuta eti taasisi kubwa kabisa...

Dhulma imejaa baadhi ya taasisi ndio maana hawaendelei, huwezi kusikia ujinga kwa watumishi wa BOT,TRA,TPA,EWURA,TCRA ,LATRA

Ila Taasisi nyingine ni dhulma wanamuhamisha mtu hawamlipi kwa ujinga wao,hao ma-HR wanaona sawa mtumishi kuhama bila ya malipo kwa vitisho eti afanye kuwahi kuripot then wanamtelekeza bila ya stahiki..

Hii dhulma inatafuna taasisi nyingi watu wanajaza madokezo ya psho hawalipwi..Sasa kuna maana gani unakuja kumlipa mtu baada ya miezi 5 ni ujinga tu.
 
Back
Top Bottom