Naomba msaada wa kujua gross na net salary ya mtu mwenye basic ya 2,192,540 Tshs

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
250
Habari za jioni wadau?

Naomba msaada wa kujua total overtime, gross na net salary ya mtu (KWA MWEZI), kwa mwenye basic salary ya 2,192,540 Tshs anayolipwa kwa kufanya saa 45 kwa wiki moja, i.e Mon-Fri (08:00-17:00) na Sat (08:00-13:00).

Lakini akatakiwa kufanya na overtime ya kila siku kwa 12 hours (11 working hrs and 1 hr for meals) per day; 7 days a week. Yaani bandika bandua.

Likizo siku 28 tu kwa mwaka.

Naomba mchanganuo wa OVERTIME, GROSS, NSSF, PAYE na NET, bila kuhusisha public holidays.
 
Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,333
2,000
Aiseee...

1. Malipo ya overtime yanatofautiana kulingana na shirika. Sijaju serikalini, maana hujasema kama ni serikakini au private.

2. Gross pia hutegemea na malupu lupu mengine, mfano nyumba, usafiri, n.k..sasa kupata gross ni lazima ujumlishe na hayo malupu lupu mengine, so wewe ndio unayajua, sisi hatuyajui hivyo ni ngumu kutaja au kukuambia gross salary yako.

3. Always NSSF ni 10% of your basic salary.

4. Kujua kiwango cha net salary, ni lazima tujue kama kuna contribution zingine zinakuwa deducted from your salary, mfano malipo ya mkopo, uchangiaji kwenye mifuko ya vyama vya wafanyakazi n.k

5. PAYE inakokotolewa soon after ku deduct passions fund, so chukua basic yako, toa pension fund, Jumlisha ma hayo malupu lupu menigne, figure utakayopata kaiingine kwenye kikokotoo kwenye website ya TRA utapata majibu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
250
Aiseee...

1. Malipo ya overtime yanatofautiana kulingana na shirika. Sijaju serikalini, maana hujasema kama ni serikakini au private...
Asante sana kwa majibu mazuri.
Kwa kifupi nahitaji kujua hiyo total overtime hours kwa mwezi itakuwa kiasi gani kwa kuangalia vyote nilivyotaja (kufanya kazi 12 hours in a day/ 7 days in a week with only 28 days of annual leave).

Assuming overtime pay na makato mengine yatazingatia sheria za Tanzania na HAKUNA MALUPULUPU MENGINE yanayoweza kuathiri gross pay na HAKUNA MAKATO MENGINE ZAIDI YA HIYO 10% YA NSSF NA PAYE zinazoweza kuathiri net pay.
 
TOTAL OVERTIME HOURS IN A MONTH & hence OVERTIME PAY.... by considering working hours and annual leave.

Huo ndio msingi wa swali.
Yaani overtime hours zitakuwa ngapi na pesa itakuwa ngapi kwa sheria za Tz.
 
Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,333
2,000
Asante sana kwa majibu mazuri.
Kwa kifupi nahitaji kujua hiyo total overtime hours kwa mwezi itakuwa kiasi gani kwa kuangalia vyote nilivyotaja (kufanya kazi 12 hours in a day/ 7 days in a week with only 28 days of annual leave).

Assuming overtime pay na makato mengine yatazingatia sheria za Tanzania na HAKUNA MALUPULUPU MENGINE yanayoweza kuathiri gross pay na HAKUNA MAKATO MENGINE ZAIDI YA HIYO 10% YA NSSF NA PAYE zinazoweza kuathiri net pay.
Au mimi ndiyo sijaelewa, maana unachokata hapo ni kupata Jumla ya overtime hours, ambazo kimsingi hata wewe unaweza ukazijua kwa kufanya simple calculation.

Kwa sababu tayari unajua overtime hrs ni 12 hours, na siku ambazo unafanya kazi overtime ni 7 days au 6 daya, sasa kwa nini usizidishe!?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
250
Au mimi ndiyo sijaelewa, maana unachokata hapo ni kupata Jumla ya overtime hours, ambazo kimsingi hata wewe unaweza ukazijua kwa kufanya simple calculation.

Kwa sababu tayari unajua overtime hrs ni 12 hours, na siku ambazo unafanya kazi overtime ni 7 days au 6 daya, sasa kwa nini usizidishe!?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Wataalamu (HR) wanajua,huwa kuna vinamba kama vile sijui 4.333 times nini, sijui vitu gani vingine....
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,050
2,000
Wataalamu (HR) wanajua,huwa kuna vinamba kama vile sijui 4.333 times nini, sijui vitu gani vingine....
Jinsi ya kupata malipo ya overtime ni hivi.
Tafuta mshahara wako wa kila lisaa limoja yaani kwa mfano mshahara wako wa lisaa limoja ni 10000.

Zidisha 10000 mara 1.5 mara idadi ya masaa ya ziada/overtime uliyofanyia kazi kwa siku za kawaida. Kisha chukua 10000 mara 2.0 mara idadi ya masaa ya ziada/overtime kwa masaa ya weekend. Kisha chukua jumla yake kwa mwezi mzima hayo ndio malipo yake.
Utaujuaje mshahara wako wa kila lisaa?

Kama ulisema kwa kawaida unafanyia kazi masaa 45 kwa wiki maana yake kwa mwezi unafanyia masaa 45x4(180) hrs. Chukua mshahara wako gawanya kwa 180 utapata mshahara wa lisaa limoja. Na malipo ya overtime haina ulipaji maalum,kuna kampuni zingine wanaichanganya kwenye mshahara wako kisha inakatwa kodi na kuna kampuni zingine wanakulipa seperate na haikatwi kodi.

Na kuna kampuni nyingine mnapatana jinsi ya kulipana overtime huwa hawatumii kabisa hesabu hizi.
Nafikiri umepata mwangaza kidogo
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,050
2,000
Habari za jioni wadau?

Naomba msaada wa kujua total overtime, gross na net salary ya mtu (KWA MWEZI), kwa mwenye basic salary ya 2,192,540 Tshs anayolipwa kwa kufanya saa 45 kwa wiki moja, i.e Mon-Fri (08:00-17:00) na Sat (08:00-13:00)...
Kuna uwezekano wa kujua netpay ya basic salary yako ila hatuwezi kujua Gross salary yako na malupulupu mengine. Angalia hapa chini kwenye attachment nimekuwekea Net salary yako baada ya kukatwa kodi na NSSF. Pesa ya overtime utajumlisha mwenyewe kwa muda wako because overtime sio kitu standard.

Screenshot_20201021-083543.jpg
 
Da Gladiator

JF-Expert Member
Aug 3, 2020
1,281
2,000
Duuh kuna watu wanalipwa pesa mingiiiiiiiii.
2M, mshahara wa miezi mitano(5) kwa mwalimu wa Diploma, miezi zaidi ya sita(6) kwa Mwalimu wa Cheti.
 
Sep 21, 2020
24
45
Aiseee...

1. Malipo ya overtime yanatofautiana kulingana na shirika. Sijaju serikalini, maana hujasema kama ni serikakini au private.

2. Gross pia hutegemea na malupu lupu mengine, mfano nyumba, usafiri, n.k..sasa kupata gross ni lazima ujumlishe na hayo malupu lupu mengine, so wewe ndio unayajua, sisi hatuyajui hivyo ni ngumu kutaja au kukuambia gross salary yako.

3. Always NSSF ni 10% of your basic salary.

4. Kujua kiwango cha net salary, ni lazima tujue kama kuna contribution zingine zinakuwa deducted from your salary, mfano malipo ya mkopo, uchangiaji kwenye mifuko ya vyama vya wafanyakazi n.k

5. PAYE inakokotolewa soon after ku deduct passions fund, so chukua basic yako, toa pension fund, Jumlisha ma hayo malupu lupu menigne, figure utakayopata kaiingine kwenye kikokotoo kwenye website ya TRA utapata majibu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kwa kuongezea tuu navyofahamu Mfanyakazi unachangia 10% na mwajiri anachangia 10%
 
Mpombote

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
1,928
2,000
Swali gumu hili japo ni rahisi kulingana na nature ya Taasisi husika mfano hapo hujasem ni Private or Government.

Maana upande wa Government ni 5% zinaenda PSSSF kuna Trade union 2% NHIF 3% hizo ni compulsory Contribution.

Na kuna PAYE pia upande wa Overtime Gorvenment haitakiwi kuzidi Masaa 50 yaani means 100 maana yanazidishwa kwa mbili na uli uzidi masaa 100 ni mpaka kibali maalumu na kinaombwa na MD wa Taasisi husika kwenda kwa Waziri husika na unyeti wa hiyo kazi pia rate hutegemea na mshahara wako,kwa kawaida weekdays unazidisha rate per hour kwa 1.5 na weekend na public holidays unazidisha rate per hour kwa 2.

Jielezee vizuri ili upewe majibu sahihi hivi vitu hutofautiana sana mfano kuna Taasisi Overtime,other benefits(Housing,Transport,Responsibilies allowance) zinaingia kama ilivyo yaani ni Non Taxable wakati kuna sehemu nimesikia ni Taxable.
 
Mpombote

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
1,928
2,000
Duuh kuna watu wanalipwa pesa mingiiiiiiiii.
2M, mshahara wa miezi mitano(5) kwa mwalimu wa Diploma, miezi zaidi ya sita(6) kwa Mwalimu wa Cheti.
Kawaida tu kuna Mashirika Mtu mwenye Darasa la Saba anakula 1.3M plus Overtime inafika hadi 2M hapo mtu ndo utajiona Lofa Sana ni vitu vya kawaida mkuu.
 
Saveya

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
1,824
2,000
Kawaida tu kuna Mashirika Mtu mwenye Darasa la Saba anakula 1.3M plus Overtime inafika hadi 2M hapo mtu ndo utajiona Lofa Sana ni vitu vya kawaida mkuu.
Kumbe darasa la saba bado wapo/wana Ajiriwa kwenye utumishi wa Umma
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,050
2,000
Kwa sasa hawaajiriwi lakini kuna wale ambao walishaingia tangu zamani.
Watafute wale walinzi wa bandarini halafu kaa nao uwalize wanaingiza pesa ngapi kwa mwezi unaweza kutoa machozi ukajiona dunia haikupendi.
Kumbe darasa la saba bado wapo/wanaAjiriwa kwenye utumishi wa Umma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom