Naomba msaada wa kitaalamu juu ya UHARAKA wa mambo yangu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,135
10,352
Habari wanabodi

Ni siku nyingine ya jumanne tulivu Hali ya hewa inaruhusu kufanya kazi hasa kwa wale waishio Kanda ya pwani.

Changamoto kubwa ni umeme hasa wengine ambao 95% ya kazi zetu zinahusiana na umeme

Nisiwachoshe,kichwa Cha habari kinajieleza,kwenu ndugu zangu wanasaikolojia, na wengine wenye changamoto kama yangu mnisaidie

Iko hivi ,binafsi Nina tatizo fulani la UHARAKA yaani Mimi kutaka vitu viende haraka haraka,

Kwa mfano nikiongozana na mtu barabarani hasa tukitembea kwa miguu mara nyingi naona kama hatembei,na mara nyingi watu kibao hunilaumu

Pia mtu akiniambia nimsubiri mahali mara nyingi tunaweza kukubaliana labda bàada ya nusu saa,lakini Mimi huwa nakwazika kuona mtu kachelewa lakini ukweli mtu anaripoti ndani ya muda husika

Yapo mengi,hata nikitongoza mwanamke huwa sipendi kuchelewa yaani inshort zisizidi siku mbili,kinyume na hapo ni kubwagana tu maana wapo wanaohisi sipo serious kwa UHARAKA wangu

Pia wengine huhisi nawachukulia poa au kuwafananisha na wale wakununua Hali ambayo tangu miaka mingi inanisumbua na kupelekea kukosa vitu sahihi

Lakini pia utendaji wa kazi ofisini kwangu,hapa sitaongea mengi,haraka zangu zimeleta manufaa kwa baadhi ya vitu ila kwa asilimia sabini nimeharibu

Mfano naagiza mzigo wa dukani kwangu ,lakini wakala anagundua mzigo wenye ubora haupo kwa wakati huo basi ananiambia kuwa labda nisubiri bàada ya siku kadhaa wiki n.k

Basi kipande hiki Cha kusubiri dah,kinanishinda basi matokeo yake unaletewa famba yaani mzigo hauna ubora kumbe ningesubiri ningepata kitu quality na bei ya chini ila Sasa

Majuto ni mjukuu.

Yapo mengi,nilinusurika ajali,kwa kulazimisha kuendesha gari ambayo fundi kadai turekebishe brake system,mi nikaona weeee usinicheleweshe nisiwahi mizunguko yangu kisa brake wakati inashika kumbe ni kwenye speed ya chini.what's happened, pengine nisingeandika kitu hii Leo

Pia,vijana wangu wa kazi nimewapunguza wengi kwa kuona hawafai ila bàada ya kutoka lile gap hunijulisha kuwa nimeshindwa kufanya maamuzi sahihi

Kitaalauma Mimi ni architecture yaani msanifu wa majengo nikiwa kijana mdogo sijisifii ila nimewahi kupata heshima na hata kipato Cha kueleweka .kwenye kazi hii
kabla sijaacha na kugeukia mishe zingine

Ila kilichokuwa kinanigharimu Kila nikikosea jambo kwenye mambo mengi ilikuwa ni UHARAKA yaani mtu anakwambia wewe unajua Tena sana tatizo umeharakisha

Haraka,haraka,haraka,yaani UHARAKA

Kuna jambo huwa najilaumu hadi Leo,Kuna mwaka nilimtafuta kijana wa kunitengenezea mashine fulani,na huyo dogo nililetewa na mshikaji mmoja akanihakikishia kuwa ni fundi mzuri,

Basi bwana dogo kafika,kaanza kazi kahangaika nayooooo,Hadi zikakatika siku mbili nikaona humu hamna fundi kwa haraka zangu nikampigia yule aliyemleta nimweleze kuwa huyu dogo hamna kitu

Jamaa alinihakikishia kuwa nimpe muda ,mi nikaona wasinichezee wanapeana michongo tu Hawa nikamtimua,lakini dogo alinambia tatizo yeye kasoma mashine za kitaliano na hizi za kichina zimetofautiana

Hivyo nimpe muda , nikamwambia aondoke tu, Cha ajabu nilileta mafundi 26 walishindwa nikaanza kuzunguka nayo Sasa kuwapelekea mafundi wengine ikawa holla mwaka ukakatika nikakata tamaa

Siku Moja my wife akaniambia Kuna kampuni Moja Iko pembeni ya mji kasikia Kuna fundi hashindwi kitu,kuhusu hizi mashine

Mie huyo haraka haraka nikaipeleka ,kufika kule hamadi nakutana na dogo yule fundi wa mwanzo Tena akiwa msafi kuliko kipindi kile yaani anatoa maelekezo tu kwa mafundi wenzie

Basi aliponiona alitabasamu hasa bàada ya kugundua nipo na ile mashine kufumba na kufumbua bàada ya masaa manne nilikabidhiwa chombo kikiwa safi nikajilaumu

Kwanini sikumpa muda,halafu kijana wa watu ni mstaarabu si mtu mwenye kujiona

Tatizo langu wanabodi matatizo yangu huwa ni yenye kujirudia,tatito ni nini?

Kitu siwezi kuficha ni kwamba nakunywa pombe Wala sijifichi

Tena mnywaji mzuri tu,nimebainisha hili ili niwape uwepesi pa kuanzia

Wenye mawazo yenye tija, ushauri mzuri mnakaribishwa

Ahsante sana.
 
Ha haaaa...
Daah, in short na Mimi pia niko almost kama wewe
- Napenda UHARAKA
yan napenda twende na muda, napenda nifanikiwe mapema, napenda nijue vitu vingi mapema, yani nikipata shida nataman niitatue mapema.

Hii ishu ilipelekea hadi mshahara nikaanza kuona hautoshi, maan ikitokea ishu ndogo naitatua mapema tena nataka iishe fasta so natumia pesa nyingi..

Lakini UVUMILIVU ndo msingi.
Nilivumilia nikapata nyumba nzuri..
Nilivumilia nikapata usafiri mzuri..

Mkuu jifunze kuvumilia
Jitoe kwenye comfort zone
Pia soma na vitabu hua inasaidia kutuliza akili
 
Ungetueleza na mengine yatu entertain.

Mfano ukitongoza kunaendaje? Je unambeba juu juu ukampige ukuni atakubali baadae?
 
MKUU hizo sio haraka ni papala. Punguza papala. Weka muda wa kulifanya jambo, hasa mambo yanayotaka maamuzi yako usiamue haraka. Jipe muda zaidi.
 
MKUU hizo sio haraka ni papala. Punguza papala. Weka muda wa kulifanya jambo, hasa mambo yanayotaka maamuzi yako usiamue haraka. Jipe muda zaidi.
 
Back
Top Bottom