Naomba msaada wa kisheria

Mwenge07

New Member
Feb 1, 2021
2
0
Mwaka 2016...mzee mmoja aitwae STIVIN anayeishi mkoa wa RUVUMA wilaya ya mbinga Dc aligongwa na gari kampuni ya SUPERFEO inayofanya safari za Mbinga to Dodoma hadi kupelekea kupoteza miguu yake yote miwili.

Jambo la kusikitisha ni kwamba Kampuni hiyo haikutoa msaada wowote kwa mzee huyo.Pia baada ya kupata unafuu wa hali yake alifungua kesi dhidi ya kampuni hiyo na akashinda MAHAKAMA ikatoa huku alipwe fidia lkn fidia iliyoamuliwa na mahakama ni kuwa alipwe Tsh .milion 12.

Ombi langu kwenu wana JamiiForums ni kwamba naomba msaada wa kisheria kuhusiana na jambo hilo.

Je, ni haki alipwe hiyo milioni 12 mtu hana miguu kwa sasa hiyo anafanyia nini.

Je, kweli Mahakama imetoa hukumu iliyo sahihi hapo?
 
Mwili wa binadamu hauna spea na hauchezewi kwa hela yoyote ile mi nijuavyo

Ngoja wanasheria waje
 
Angetakiwa kukata rufaa kupinga kiwango cha pesa na sio kulalamika Sheria ipo wazi usipolizika na maamuzi ya mahakama fulani unaymtakiwa ukate rufaa tu
 
Back
Top Bottom