Naomba msaada wa kisheria kumwongoza dada yangu baada ya kunusurika kubakwa

Bunguabongo

Member
Jan 12, 2011
27
22
Ndugu wanajamii wenzangu wapenda haki, naombeni ushauri wenu kumsaidia mdogo wangu aliyenusurika kubakwa na vijana watatu.

Kwa kifupi suala liko hivi, mdogo wangu alitumwa kwenda mashineni kusaga unga akiwa na baiskeli (nafikiri mnafahamu mazingira ya vijijini), sasa wakati anarudi nyumbani akakuta kizuizi njiani maeneo ya porini. Alivyoteremka kuondoa kile kizuizi ghafla akavamiwa na wavulana wanne ambao inaonekana walikuwa wamejificha. Mdogo wangu akakamatwa na kuanza kuvutwa kuelekea porini na walivyofika huko porini wakaanza kumgawana katika harakati za kumbaka. Bahati nzuri sauti yake ya kilio ilisikika na mpita njia mmoja aliwakurupua hao vijana na kumwacha mdogo wangu akiwa analia akitokea porini. Bahati nzuri mdogo wangu alikuwa hajafanyiwa kile walichotaka kukifanya.

Taarifa zilifika ofisi ya mtendaji wa kijiji na watuhumiwa baadhi wakakamatwa na kuwekwa ndani hapo ofisi ya mtendaji wa kijiji. Cha kusikitisha ni kwamba watuhumiwa wale walidhaminiwa hapo ofisi ya mtendaji wa kijiji bila ridhaa ya mlalamikaji. Mpaka sasa baba mzazi wa mlalamikaji ameomba msaada wa polisi kwa hiyo wadhamini wawili wako ndani polisi. Swali ni je, sheria inasemaje katika suala kama hili na nifanye nini katika kumsaidia mdogo wangu huyu ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Tatu ili aweze kutendewa haki na utaratibu mzima wa kufungua kesi.


Ushauri wenu utakuwa na msaada mkubwa sana ktk kumsaidia mdogo wangu na wadogo zetu wengine wanaotutegemea. Kulipeleka suala polisi niliwashauri wazazi wangu kwa njia ya simu maana hata mimi niko mbali na nyumbai.
 
Pole sana.
Ninajisikia fahari kwa ujasiri wako wa kutaka kumsaidia mdogo wako bila stigma.
Hili linakuwa shambulio la aibu. Hebu google human legal rights center, utapata namba yao. Watakupa ushauri na msaada wa kisheria bure.
Nashukuru sana kwa niaba yangu mwenyewe, im so proud. Otherwise kuwa karibu na mdogo wako kwa simu. Atakuwa na uoga mwingi lakini baada ya ushauri wa wanasheria atajisikia vizuri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom