Naomba msaada wa kisheria katika hili suala langu kudhulumiwa pesa zangu za upatu

mosktear

Member
Nov 9, 2014
7
0
Tulikua tunacheza mchezo wa kupeana hela (upatu) wa 500k kila mwezi ila baada ya mizunguko kadhaa kuisha kuna ikafika zamu yangu kupokea ila katika washiri, mshiriki mmoja akaomba atanipa mwezi unaofwata kwani amekwama kutokana na matatizo yanayo mkabili.

Nikamwelewa lakini tokea pale ni miezi 6 sasa kila nikimuuliza anaishia kunipa kalenda kwamba nitakupantakupa na siku zinaenda, nafikiria kwenda kwenye vyombo vya dola (polisi) ila sinaufahamu wowote kuhusu kesi kama hizi naomba elimu kwa wanaofahamu nitumie njia gani niweze pata haki yangu
 
Kimsingi tafsiri au dhana za vikundi hivyo ni kukwamuana au kusaidiana Kama halipo katika makubaliano ya kimkataba jambo la awali unalopaswa kulifanya ni kwamba utoe taarifa kwa uongozi wa kikundi hicho au mchezesha kikundi hakina uongozi alishughulikie.

Pili kama jitihada hizo zitakwama nenda kwa wakili yeyote aliye jirani na wewe ili amuandikie "Demand note" na atapewa siku kadhaa kumtaka alipe kiasi hicho unacho mdai, akiwa ni mtu mwenye busara atalipa katika mazingira hayo.

Lakini ikumbukwe kwamba Mtu huyo unaye mdai atakuwa na wajibu wa kulipa pesa hiyo ikiwa tu katika mzunguko wake alipokea pesa iliyokuwa jumuishi na mchango wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom