Habarini wana JamiiForums,
Natumaini mu wazima rejea kichwa cha habari hapo juu. Mimi ni kijana wa chuo ninaejihusisha na biashara ndogondogo kama kuuza karanga nyekundu ,visheti, kashata na karanga za mayai.
Msaada ninaomba ni upande wa karanga za mayai. Kuzipika najua ila kila nikipika zikikaa wiki zinabadirisha ladha inabadilika.
Hivyo, naomba ushauri wa jinsi ya kutengeneza ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

Umewahi kupitia maelezo haya
mahitaji ya awali kabla ya kuanza kukaanga karanga za mayai.
1. Sukari kiasi
2. Unga wa ngano kilo 1 moja na nusu.
3. Karanga kilo 1
4. Mayai 3
5. Mafuta ya kupikia kiasi kulingana na mchanganyiko wako.
Namna ya kutengeneza
a. Pasua mayai ,changanya mayai na sukari kisha koroga katika chumba kimoja.
b. Hatua ya pili chukua unga wa ngano kisha changanya na mchanganyiko namba (a) yaani mchanganyiko wa mayai na sukari.
c. Weka mafuta katika sufuria kisha injika motoni. Lakini hakikisha moto hauwi mkali sana. Ukiwa mkali sana utasababisha karanga kuungua sana na kupoteza radha.
d. Koroga mchanganyiko huo taratibu ili kuondoa kugandamana kwa mchanganyiko huo wa karanga pamoja na unga wa ngano. Fanya hivyo kila baada ya dakika kadhaa.
e. Ukiona zimeanza kubadilika rangi onja kwa kujiridhisha kama kweli zimeiva.
f. Zikisha iva ziepue kisha weka katika chombo kisafi ili zipoe.