Naomba msaada wa JF doctors.

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam! Wakati nakojoa (haja ndogo) nasikia maumivu makali sana,na rangi ya mkojo ipo kama ya brown! JF doctors naomba msaada wenu. Asante.
 
mzee kachek fasta sana,yawezakua umepata STD.kuchelewa kupata tiba kunaongeza uwezekano wa ugonjwa kuua kabisa viungo vyako vya uzazi
 
una kunywa maji kwa wingi?kama ndio badi inawezekana ikawa UTI,zo mm si Dr lkn najua kutumia vyoo watu wengi pia huleta magonjwa mlipuko,nenda hsp watakupa dawa,pole sana wahi mapema kabla halijawa tatizo kubwa.
 
kunywa maji mengi - mwili uko dry huo - lazima mkojo wako uhakikishe uko mweupe - kama maji masafi - siyo kama maji ya bomba machafu ya ruvu................ pia jicheki kama unakula chumvi nyingi ........... otherwise kama walivyoshauri wengine - nenda kapime mkoja hospital
 
Asanteni wakuu. Maji nakunywa kawaida. Wakati mwingine nakunywa mengi,wakati mwingine kidogo. Nimeenda hospitali na daktari kasema tatizo linaweza kua limesababishwa na kuchangia vyoo,maji yasiyo safi au kuambukizwa kutokana na tendo la ndoa. Nimepewa dawa,nimeshaanza kunywa na zimeshaanza kufanya kazi,kwani sasa nikikojoa sisikii maumivu na mkojo umeanza kurudi katika rangi yake ya kawaida. Asanteni sana kwa ushauri wenu.
 
kaka...peku nini?
 
QUOTE=hashycool;kaka...peku nini?

Kaka iyo ni moja ya sababu iliyotolewa na daktari. Mimi sipo kwny Pekupeku Stars. So iyo si sababu ya mimi kupata tatizo ilo. Cheki pia na sababu zingine. Asante.
 
Salaam! Wakati nakojoa (haja ndogo) nasikia maumivu makali sana,na rangi ya mkojo ipo kama ya brown! JF doctors naomba msaada wenu. Asante.
UTI!!! wacha mchezo mchafu. au bado hujatahiriwa? nenda hospitali kapime lakini la muhimu zingatia usafi hasa wa chupi, tumia maji moto uendapo haja kubwa na ndogo kujisafisha. Inaweza kukusaidia pia. kama uko mahala hakuna maabara ya maana kula vitunguu swaumu kila siku asubuhi na jioni vipunje 3 kwa wiki moja
 
Salaam! Wakati nakojoa (haja ndogo) nasikia maumivu makali sana,na rangi ya mkojo ipo kama ya brown! JF doctors naomba msaada wenu. Asante.

Huna sababu ya kuwa na shaka kuhusu majibu ya kutisha niliyoyasoma.
Mkojo huchujwa katika figo, na hupitia mjia ya mkojo kutoka. Maumivu yatokanayo yanaweza kuwa yamesababishwa na mambo anwai. Si rahisi kufikia conclusion kwa maelezo yako mafupi. Inabidi tupate historia fupi ya tatizo na ukweli utokanao. Mkojo kuwa wa njano yaweza kuwa upo concentrated sana, au kuna excess bilirubin breakdown in the body n.k. Maumivu yawezasababishwa na mambo mengi ikiwa pamoja na maradhi kama Gonnorrhea n.k. Napenda kukuhakishia kuwa maumivu ya mkojo si dalili za uwepo wa ngoma moja kwa moja.
Kwa ushauri wangu, inabidi uonane na Daktari ili apate history yako vizuri na nina hakika atakutuma vipimo vya maabara to rule out other factors which could have similarity in presentation. Hakuna jibu la mkatao na sahahihi unaweza kupata hapa bila vitu hivyo viwili.
 
Back
Top Bottom