Naomba msaada wa haya matatizo ya akili

Step by step

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
1,249
1,277
Habari ndugu wajumbe.

Kuna hali nimekua naipitia inanivuruga kabisa.
Umri wangu ni miaka 35 jinsia ni ME, shida ni kwamba ninapokua na ratiba mpya au jukumu jipya au taarifa ya kushtua ninapoipata tu afya inayumba kwa dalili zifuatazo.
1. Sitapata usingizi yani usiku hadi panakucha.
2. Napata kichefuchefu, mate yanajaa mdomoni.
3. Naweza pata dry throat, koo linakauka, nameza mate kwa tabu.
4. Tumbo linavuruga, naharisha.
5. Mwili unaisha nguvu, nakua dhaifu kabisa.

SULUHU ambacho nimekua nikifanya ni kutafuta dawa za usingizi kidogo tu mara nyingi huwa natumia vitamin PHAMACTIN (nikinywa mills tano tu) inanipa usingizi. Nikilala nikiamka akili inakua imesahau ile taarifa hivyo nakua sawa.

Naweza pewa ratiba ya safari, hiyo hali ya kuumwa inanivaa nakua dhaifu lakini ikatokea nikaambiwa safari imeahirishwa baada ya muda mfupi nakua normal.

Ni kama ain fulani ya fear of unknown. Je, kuna dawa za kumeza ili ku stabilize mood? Dawa ambazo ukimeza huogopi kitu, una uwezo wa kufanya chochote bila mshaka maana ni kama akili yangu inatanguliza mabaya kwenye rtiba mpya.

Njua hapa pana wataalam wengi tafadhali nombeni msaada maana ladh ya kuishi inapotea
 
Kama umejigundua mwenyewe probably hio sio mental health problem, wagonjwa huwa hawakubali kwamba wanaumwa na ni moja ya criteria ya ku diagnose mental problems.

Nakushauri uende hospital kule utafanyiwa examinna na vipimo vitakavyo toa majibu sahihi na suluhisho la tatizo lako chief!!!
 
Same to me br...Yan huwa nakuwa very weak...Kama mgonjwa wa malaria..
 
Kama umejigundua mwenyewe probably hio sio mental health problem, wagonjwa huwa hawakubali kwamba wanaumwa na ni moja ya criteria ya ku diagnose mental problems. Nakushauri uende hospital kule utafanyiwa examinna na vipimo vitakavyo toa majibu sahihi na suluhisho la tatizo lako chief!!!
Shukrani sana mkuu kwa kujali. Yani taarifa nyingine inakua ni ya kawaida tu wala sio ya kushtua, naipata naenda zangu kulala nikipanda kitandani usingizi hauji na tumbo linavuruga kitu ambacho hata sikielewi
 
Same to me br...Yan huwa nakuwa very weak. Kama mgonjwa wa malaria..
Mwenzangu unatumia njia gani kujinusuru? Mimi kuna baadhi ya ratiba na safari nimeamua kuji exclude tu. Yni ni ka hofu flani ambako kanakuja automatically. Ni kama kin nguvu flani inakuvut unajikuta ushavurugwa. Siamini kama ni ushirikin na sitaki hta kufikiria hivyo
 
Kuna muda huwa natumia music Kama tiba ya kusahau na kuipotezea hofu
Mwenzangu unatumia njia gani kujinusuru? Mimi kuna baadhi ya ratiba na safari nimeamua kuji exclude tu. Yni ni ka hofu flani ambako kanakuja automatically. Ni kama kin nguvu flani inakuvut unajikuta ushavurugwa. Siamini kama ni ushirikin na sitaki hta kufikiria hivyo
 
Back
Top Bottom