Naomba msaada toka kwa raisi wangu mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete


O

optimistic1

Member
Joined
Jun 10, 2013
Messages
5
Likes
0
Points
0
O

optimistic1

Member
Joined Jun 10, 2013
5 0 0
RAISI WANGU MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Raisi wangu naomba nikupe pole kwa majukumu ya kila siku ya kitaifa, naona misukosuko mingi inajitokeza Tanzania mfano Mtwara Mungu azidi kuisaidia Tanzania na kuidumisha amani.
Raisi wangu nimekua ni mtu ambaye nafuatilia kujua wewe ni raisi wa namna ipi, nimeridhika na raisi wangu. Hata leo najitokeza kuadika ujumbe huu kwako raisi wangu nikiomba msaada wako wa dhati.
Mimi ni kijana ninayetoka katika familia ya kimasikini, kusoma kwangu kulikua kwashida sana. Namshukuru mungu nimemaliza elimu yangu ya juu ktk chuo kikuu kimoja hapa nchini mwaka mmoja uliopita. Katika mlolongo wa shule nilizo soma ni zile shule za wengi ambazo masikini wengi wanaweza kumudu. Katika maisha yangu nimekua nikiamini kua elimu ndio ukombozi wangu katika kujikwamua katika ugumu wa maisha, pia bado naamini hivyo kwani kwakusoma kwangu nimeondoa ujinga na kugain vitu vingi ambavyo ni msaada kwangu.
Raisi wangu sijaona njia ambayo ningeweza fikisha ombilangu kwako zaidi ya hapa nilipo tumia pia naamini lazima maombi yangu yangu yatafika kwako.

MAOMBI YANGU KWAKO RAISI WANGU
Raisi wangu naipenda nchi yangu nabado sijafikia pointi ya kuilaumu nchi yangu. Ninasifa za kuajiriwa na kufanya kazi, lakini bado nashuudia watu wakiajiriwa na mimi nikiendelea kuapo mitaani. Raisi wangu naamini kua wewe ndio TOP katika nchi hii, naomba unisikilize mimi mtanzania ninaye omba msaada wako siku hii ya leo, ninaamini kwa msaada wako raisi wangu wakati wowote na saa yoyote naweza pata ajira katika nchi yangu ya Tanzania.
RAIS WANGU NAOMBA UNISAIDIE MWANANCHI WAKO NIWEZE PATA AJIRA.
Laiti ningekua na uwezo ningeweza fika ikulu au ningeweza simamisha msafara wako kwaajiri ya kuomba msaada wako, na wengi waweza ona nimekurupuka na nimefanya ujinga ukweli ni kwamba nimejaribu kutafuta kazi kwa kadri ya uwezo wangu wote bila hata MAFANIKIO. Raisi wangu sikia kilio na ombi langu.
Raisi wangu naomba kwa Mungu ujumbe huu ukufikie kwani naamini ujumbe huu ukifika kwako lazima raisi wangu utanisaidia mwananchi wako nisiyekua na msaada wowote. Pia nakumbuka umeisha wasaidia watu wengi sana katika nchi yako, nitazame na mimi leo hii.
Raisi wangu nashukuru sana kwa yote , pia naamini kua ujumbe wangu utakufikia na msaada nitaupata toka kwako.

MWISHO
Namuomba Mungu wangu azidi kukupa afya njema na maisha marefu zaidi, pia Mungu azidi kukuzidishia hekima katika kuliongoza taifa la Tanzania.


optimistic1980s@gmail.com
 

Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044