Naomba msaada tafadhali, kuondoa SMS za push

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
195
Helo wanaJF,

Naomba msaada wa jinsi ya kuondoa meseji za mtandao wa push kwenye simu ya Vodacom au hata zingine, maana zinaniletea kero. Utakuta wakati fulani unajaza vocha ya sh.500 kwa mfano, halafu baada ya hapo zinaingia hata sms 3 ambazo kila moja wanakata sh.150 na matokeo yake unakosa mawasiliano.

Nimejaribu mara kadhaa bila mafanikio, nilielekezwa kutuma sms yenye neno ONDOA kwenda 15500, kama kuna namna nyingine naomba msaada.

Thanks
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom