Naomba msaada: Natakiwa kupewa stahiki gani endapo mwajiri ananipunguza kazini?

Mkataba wako wa kazi unasemaje?
Lakini kwa haraka-haraka utalipwa unused leave days ukafie mbele. Na hivi Mr. Kuku kimenuka sijui utaenda kuwekeza wapi.
 
Kuna utata..mwajiri alijua mapema atakachofanya badaye ndiyo maana hakukupa mkataba na inaonekana ndiyo njia yake anayotumia sana kukandamiza upande mmoja.

Hapo angalia ustaarabu wako wala usibishane na mtu mana yatakuja mengine halafu pia kuna kesho pia kwa kampuni hiyohiyo.
 
Kuna utata..mwajiri alijua mapema atakachofanya badaye ndiyo maana hakukupa mkataba na inaonekana ndiyo njia yake anayotumia sana kukandamiza upande mmoja.

Hapo angalia ustaarabu wako wala usibishane na mtu mana yatakuja mengine halafu pia kuna kesho pia kwa kampuni hiyohiyo.
Asingeweza kupewa mkataba juu ya mkataba (maana alikua nao tayari, Happ angepewa Addendum na hiyo promotion). Akafuge samaki tu hamna namna
 
Nkushauri hivi: siku ya kwenda kwenye consultation (maana itakuwa kati yako na mwajiri wako) nenda na mtu anayejua sheria za kazi (anaweza kuwa mwanasheria wako*) ambaye utakuwa umemweleza issue yako na kuielewa vizuri ili akusaidie kwenye 'negotiation'. Vinginevyo, waajiri wengi ni wajanja. Kwenye mkutano kama huo wao watakuwa na mwanasheria wao na wewe ukienda kichwa kichwa unakuta unatoka kichwa kichwa pia.

Baadhi ya waajiri wanakwambia 'verbally' kwamba "kwenye consultation unaweza kuja na mtu anayeweza kukushauri ambaye ni lazima awe mfanyakazi" lakini kwenye barua unayopewa wanataja tu kwamba "unaweza kuja na mtu anayeweza kukushauri".

Advantage ya kwenda na mtu anayejua sheria ni kwamba ataweza kumuuliza mwajiri maswali ambayo mtu asiyejua sheria za kazi hawezi kuuliza na inaweza ikaleta nafuu fulani kwa upande wako as far as kupunguzwa kazi is concerned maana wakati mwingine kupunguzwa kazi kunaweza kuangukia kwenye 'unlawful retrenchment'. Sasa ili kujua which is which mpaka uwe na mtu anayejua sheria za kazi Tanzania ndiye anayeweza kukusaidia kwenye negotiation. Kwa leo niishie hapa.
 
Embu muone kwanza mwenyekiti kuhusu hili na umwambie huku hali mbaya makampuni meeeeeengi yamepunguza wafanyakazi kwa kigezo cha kampuni inajirndesha kwa hasara
 
Hapana wenye kampuni ni makaburu (wazungu wa south afrika) ila MD ni muingereza na HR ni MUHAYA
We endelea kulalama humu badala ya kutafuta fursa za kupata pesa. Halafu Kuna mtu anadai Kuna kitu inaitwa **unlawful retrenchment**? Seriously?? Plz tumia trade unions Kama zipo. Vinginevyo kwenye negotiations muwe wapole kuomba mwajiri awape mishahara angalau miwili au mitatu na awaachie kadi za bima za afya angalau kwa mwaka mmoja (mkijidai vidume mtakosa yote)
 
Asante kwa ushauri wako mkuu,
Ila kuhusu kwenda na mwanasheria tumeruhusiwa kufanya hivyo, ila kwa wakati nilionao kwakweli sitaweza kumpa pesa za gharama atakazohitaji ili niweze kwenda nae
Utajutia hili mzee hayo mambo ya CMA lazima upate mtu mwenye uelewa nayo ili awabane kwenye sheria.
 
Asante kwa ushauri wako mkuu,
Ila kuhusu kwenda na mwanasheria tumeruhusiwa kufanya hivyo, ila kwa wakati nilionao kwakweli sitaweza kumpa pesa za gharama atakazohitaji ili niweze kwenda nae
Hata kama siyo mwanasheria anaweza kuwa mtu mwenye uelewa wa mambo na mafao ya wafanyakazi wanaopunguzwa kazi (kupunguza operational costs na siyo kukosa sifa za kufanya kazi). Au unaweza kwenda kwa mwanasheria akupe ushauri maeneo ya kuuliza maswali au namna nzuri ya ku'negotiate' mafao (if there are any). Yaani, kwa kifupi nenda ukijua unachotakiwa kujua na kupata, otherwise baada ya kuwa 'laid off' ndipo utakapojua na kuanza kujisikia vibaya kwa nini hukutafuta ushauri kwanza. Hopefully, ulikuwa na permanent contract na kama hivyo ndiyo, then premature termination of contract must comply with labour laws.
 
Pole sana hii imewahi nikuta miaka ya 20

Hakuna sheria ya hovyo Tanzania kama sheria ya kazi nasharuri Moderator waanzishe forum ya kazi haya mambo yanasumbua sana

Sheria ya kazi inamtaka mwajiri wako akulipe 1/4 ya mshahara wako *miaka uliofanyia kazi kama kakuachisha kazi mwenyewe yaani mfano mshahara ni milioni 1 maana yake utalipwa 250,000mara idadi ya miaka uliofanyia kazi katika kampuni hiyo pia kama ni Contract ambayo sio permanent utalipwa mshahara wa miezi mitatu mchezo umeishia hapo

Hapo sasa itategemea na mwajiri wako anasemaje akiamua kufata hizo sheria za kazi umeumia bro hapo hamna kitu

Anza kutafuta kazi sehemu nyingine

Sheria za kazi ni za kijima sana za miaka ya 1990 hazisaidi katika ulimwengu wa leo

Me yameshawahi nikuta ya hivyo miaka ya 2009 hivi vilikuwa vichekesho vitupu
 
Kwanza huna haja ya mkataba mwingine ilihali tayari unao mkataba wa awali hizo documents za promotion na allowance zilizoongezwa xitatumika kama kielelezo wakati wa kuvunja mkataba
 
Back
Top Bottom