Naomba msaada, nataka kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya basi la Dar Lux

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
389
Habarini za mchana wakuu,

Kama nilivyoandika hapo juu naitaji msaada wa kisheria kuhusu hili bus. Nina ndugu yangu ni mgonjwa kuna dawa huwa anatumia inamsaidia, hii dawa sehemu nilipo kuipata ni mtihani kidogo hivyo mara nyingi naiagiza Dar sababu kule nina mwenyeji na huwa ananitumia nilipo.

Tatizo mzigo umepelekwa Shekilango tarehe 9/4/2020 kwa maana unaondoka Dar tarehe 10/4/2020 halafu mimi napokea tarehe 11/4/2020, lakini toka bus litoke huko halijafika mpaka leo na ukienda ofisini kwao hawana majibu ya kueleweka zaidi wanasema bus limeharibikia Singida, huku hali ya mgonjwa inazidi kuchange na dawa imekwama kwenye bus lao imebidi leo niagize tena kwa usafiri mwingine.

Mpaka sasa hawana majibu ya kueleweka nafikiria hata kuwapeleka mahakamani kama nitapata muongozo mzuri wa kisheria ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye tabia kama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa wamelewa sifa, wamekua wazinguaji sanaaa, lawama juu yao zimezidi..
Hawajali wateja kbsaa...ukipata hio chance ya kuwabananisha usisitee,

Japo kuna inshu waweza ukutane nayo.
"Kwa nn utumie njia ya Basi?"
 
Kama basi limeharibika kweli huna namna ya kuishinda hiyo kesi, ni nje ya uwezo wao.

Halafu kwenye receipt kunakuwa na terms and conditions, zipitie uone kama una advantage kisheria.

Ushauri: Jiwekee reorder level, kwamba kikibaki kiasi kadhaa cha dawa agiza, ili hata ikitokea emergency ya kuchelewa unakuwa bado una mzigo au unaweza kufanya maamuzi mengine bila kuathiri hali ya mgonjwa. Usisubiri mpaka dawa iishe.
 
Duh Kumbe ndiyo michezo yao kwa kweli inabidi wajitafakali kwani mabasi yao yanaharibika sana
 
Hawa jamaa wamelewa sifa, wamekua wazinguaji sanaaa, lawama juu yao zimezidi..
Hawajali wateja kbsaa...ukipata hio chance ya kuwabananisha usisitee,
Japo kuna inshu waweza ukutane nayo.
"Kwa nn utumie njia ya Basi?"
Naukweli unatafuta usuluhishi wa kisheria nakati jambo unalofanya ni batili kisheria ....serikali ilitangaza kuhusu kutotuma mizigo kwenye mabasi inatakiwa kampuni iliyosajiliwa kisheria sababu ya hiyo huduma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama basi limeharibika kweli huna namna ya kuishinda hiyo kesi, ni nje ya uwezo wao.

Halafu kwenye receipt kunakuwa na terms and conditions, zipitie uone kama una advantage kisheria.

Ushauri: Jiwekee reorder level, kwamba kikibaki kiasi kadhaa cha dawa agiza, ili hata ikitokea emergency ya kuchelewa unakuwa bado una mzigo au unaweza kufanya maamuzi mengine bila kuathiri hali ya mgonjwa. Usisubiri mpaka dawa iishe.
Sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom