Naomba msaada nataka ku-reopen kampuni ya mzee wangu. Nifanyeje?

Jumjum kapo

Member
Oct 17, 2022
32
86
Kama Title inavosema

Nimekua Katika familia ya mzee mwenye uwezo kidogo lakini alifanikiwa kufungua kampuni kubwa iliyofanya ujenzi wa kazi mbali mbali miradi mikubwa.

Lakini nimemaliza chuo sasa nataka kuendeleza Ile kampuni lakini sijui nianzie wapi maana imekua domant kwa muda mrefu sana naombeni msaada au ushauri nifanyeje kama inawezekana?
 
Status yake nikitaka kufahamu nafanyaje?
Chukua TIN ya kampun. Nenda TRA mkoa uliopo. Utapata mkeka wa kampuni.
Suala unaweza kupata uhafuen wa nini na kivipi ni lugha yako na uelewa.
Zingatia usiende ofis za mamlaka kiujuaji wakaingiza details za maden kwenye mfumo, utalia.
Au tafuta tax consultant utapata mwanga. Lugha uloanza nayo nahis una kimeo cha hatari.
 
Kupokea Tender za ujenzi
Hapo sasa unatakiwa uje kivingine,dunia ya sasa ipo kwenye mitandao,kwanza fungua accounts za biashara hiyo kwenye mitandao ya kijamii ,pili tengeneza vipeperushi na business card ya biashara yako,brand biashara yako iwe kwenye usafiri au nguo utakazovaa kazini ziwe za jina la kampuni yako,weka discounts kwa kila bidhaa,last one good customer care..
 
Kama Title inavosema

Nimekua Katika familia ya mzee mwenye uwezo kidogo lakini alifanikiwa kufungua kampuni kubwa iliyofanya ujenzi wa kazi mbali mbali mirador mikubwa

Lakini nimemaliza chuo sasa nataka kuendeleza Ile kampuni lakini sijui nianzie wapi maana imekua domant kwa muda mrefu sana naombeni msaada au ushauri nifanyeje kama inawezekana??
Fuata hatua hizi:

1. Chukua TIN hiyo ya kampuni ya mzee wako, nenda TRA omba upewe ripoti kamili ie Tax position ambapo itaonyesha taarifa zote muhimu za madeni na malipo na taarifa zipi utatakiwa kuwasilisha

2. Pia inakubidi ujue TIN binafsi ya mkurugenzi mmojawapo kama ni mzee wako nk ili uweze kuupdate files kwn mfumo wa ss ni tofauti na wa zamani ili uweze kutengeza e-filling account ya kampuni

3. Nawe binafsi uwe na TIN yako ambayo ndani ya mfumo wa akaunt ya e-filling ya kampuni utajiappoint kuanza kuwasilisha ripot mbalimbali ambazo utapewa mwongozo TRA

4. Kama huna elimu juu ya masuala ya kodi na kampuni tafuta wataalam ie mhasibu au tax consultant akusaidie ila hii kuna gharama utalipa

5. Upande wa BRELA kama pia hujui ku-update taarifa za kampuni hy, pia tafuta wataalam kurahisisha mambo
 
Chukua TIN ya kampun. Nenda TRA mkoa uliopo. Utapata mkeka wa kampuni.
Suala unaweza kupata uhafuen wa nini na kivipi ni lugha yako na uelewa.
Zingatia usiende ofis za mamlaka kiujuaji wakaingiza details za maden kwenye mfumo, utalia.
Au tafuta tax consultant utapata mwanga. Lugha uloanza nayo nahis una kimeo cha hatari.

Haha Vimeo muhimu boss
 
Kama Title inavosema

Nimekua Katika familia ya mzee mwenye uwezo kidogo lakini alifanikiwa kufungua kampuni kubwa iliyofanya ujenzi wa kazi mbali mbali miradi mikubwa.

Lakini nimemaliza chuo sasa nataka kuendeleza Ile kampuni lakini sijui nianzie wapi maana imekua domant kwa muda mrefu sana naombeni msaada au ushauri nifanyeje kama inawezekana?
Kama mzee yupo muulize kama aliandika barua ya kusimamisha biashara? Kama siyo jaribu kufungua kampuni nyingine au mfuate kiongozi wa tawi la karibu la TRA ujadiliane naye. Maana kama hakuandika barua watakukadilia kodi ya kipindi chote mpaka leo!
 
Brela pia kuna ada ya return ya mwaka, ni ndogo lakini inazaa kila mwezi mpaka utaishangaa! Kama hakuna ulazima fungua kampuni nyingine.
 
Kama mzee yupo muulize kama aliandika barua ya kusimamisha biashara? Kama siyo jaribu kufungua kampuni nyingine au mfuate kiongozi wa tawi la karibu la TRA ujadiliane naye. Maana kama hakuandika barua watakukadilia kodi ya kipindi chote mpaka leo!
Naomba nijuze kama ulifungua kampuni hukufanikiwa kuiendesha kwa muda mrefu bira kutoa taarifa TRA then unataka kufungua nyengine je itawezekana na je utapotaka kwe da kutafuta Tin number taarifa za awali si zitaonesha teyar unayo Tin hapo inakuaje mkuu?
 
Uzi bora kabisa...

Free consultations....ndio raha ya JF.

Mimi pia nimepata shule ya bure kwenye mambo mengi sana hapa kwa muda wote toka kutambua uwepo wa mtandao huu.
 
Kama mzee yupo muulize kama aliandika barua ya kusimamisha biashara? Kama siyo jaribu kufungua kampuni nyingine au mfuate kiongozi wa tawi la karibu la TRA ujadiliane naye. Maana kama hakuandika barua watakukadilia kodi ya kipindi chote mpaka leo!

Ipo nyengine aliandika barua ya kusimamisha kazi.
 
Ipo nyengine aliandika barua ya kusimamisha kazi.
Alikuwa anawasilisha ritani kama inavyotakiwa kisheria baada ya kuandika barua!?
IMG_20220512_103535_762.jpg
 
Back
Top Bottom