Naomba msaada juu ya matumizi ya ruzuku(captation grants) 50% kutumika katika ununuzi wa vitabu vya kujifunzia na kufundishia, maana mkuu wa shule yetu anadai 50% ya ruzuku bado serikali haijatuma na hatujui ni lini pesa hiyo itatumwa. Je shuleni kwenu mnafanyaje maana tunaogopa matumizi mabaya ya pesa za shule. Tangu mwezi januari hatujanunua vitabu na shule haina vitabu vya kutosha. Hapa chini naambatanisha picha juu wa waraka wa elimu na matumizi ya ruzuku hiyo. View attachment 341438