Naomba msaada kwa wastani gharama za ufundi wa nyumba ya vyumba 4

f_m

Member
Sep 19, 2017
61
125
Wadau,

Naomba msaada,

Kwa wastani gharama za ufundi wa nyumba ya vyumba 4 kwa standard ya kawaida kuanzia kwenye kupandisha ukuta hadi kukamilisha lenta, je gharama za ufundi uwa ni shilingi ngapi kwa wastani au kuanzia ngapi mpaka ngapi?

Msaada plz wanajamvi
 
msigwa2018

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
257
500
Inategemea na eneo unalojenga, umbali wa upatikanaji wa maji, bei ya tofali na gharama za mafundi zinatofautiana pia wapo wenye ghrama sana na wapo wa kawaida pia hujaelelza unataka mfumo gani wa nyumba na unatumia tofali au block
 
Sammo Hung

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
1,140
2,000
Baadhi ya wachangiaji wameshindwa kumuelewa mleta mada anachokitaka, gharama za ufundi ndio zinazohitajika yani materia anayo, kiwanja anacho, na kila kitu kipo sasa gharama za FUNDI kujenga hiyo nymba ya vyumba vinne ni kiasi gani.
Sina uzoefu na mambo ya ujenzi ila nimejaribu kudadavua ili wajuzi wa haya mambo watoe jibu sahihi kulingana na matakwa ya mleta mada.
 
byembalilwa

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
1,899

eneo alipo kwabza
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,268
2,000
Milioni 8 ni msingi tu
Milioni nane inatosha kabisha.Lakini utakuta mtu anakwambia milioni Thelasini (30)
Inategemea na eneo unalojenga, umbali wa upatikanaji wa maji, bei ya tofali na gharama za mafundi zinatofautiana pia wapo wenye ghrama sana na wapo wa kawaida pia hujaelelza unataka mfumo gani wa nyumba na unatumia tofali au block
Mmeulizwa GHARAMA ZA UFUNDI.

f_m huku uswahilini tunahesabiana kwa tofali. Tofali moja 250-400. Kwahio kama nyumba itakuwa matofali 3000 hapo ni 3000*400=1,200,000.
 
mamenrevy

JF-Expert Member
Jun 9, 2014
585
500
Msingi kuchimba na kujenga wakikugonga sana 800,000/= Kuinua Boma 2,000,000/= Renter 1,000,000/= Hivyo Ghalama zita kuwa kati ya 3.5m -5m.

Chini ya 3.5m Kazi itakuwa hovyo zaidi ya 5m umepigwa.
 
Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
629
1,000
kama una muda wa kusimamia tafuta mapipa ya maji mtu akujazie maji umlipe kivyake, nunua cement mtu afikishe saiti mlipe kivyake, nunua mchanga weka hapo saiti. Kwenye ufundi kama mdau alivyosema hapo juu huwa tunahesabu tofali kuanzia 250 - 500. hiyo 250 ni laini za chini mpaka laini ya dirisha linapoanza yaani laini ya nne. Kuanzia hapo ni maelewano wewe na fundi kwa laini inayoongezeka lakini mara nyingi haizidi tshs. 500 kwa zile laini 2/3 juu ya linta. kwa hiyo utakua na kazi kila siku ya kuhesabu tofali fundi alizojenga then unamlipa basi.

Kama huna muda elewana tu na fundi kwa kazi yote halafu unakuwa unamlipa kwa kukladiria cha msingi usimlipe zaidi kuliko kazi aliyofanya. na hapa hamna fomula ni wewe tu na sound zako.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,336
2,000
Tukumbuke tunaongelea bei za wakati wa malaika sio zile za Mangungu enzi zilizopita. Sasa hivi nafasi ya kujadili punguzo la bei kubwa sana. Kazi chache.

Kwani bado mbaona utitiri wa nazi kwenye njia panda? Au yale matambiko ya kuchinja mifugo?
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
7,749
2,000
Had lenta na koz 3 juu mpe 1.5m,hyo ndo standard ingawa mim tulishuka had 1.3m maana fund alikua na njaa sana,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom