Naomba msaada kwa wabunge swali langu hili bungeni

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
naomba sana msaada kutoka kwa wabunge kutuulizia bungeni swali lifuatalo kuhusu mtumishi wa serikali au waziri kuacha ofisi ya wananchi na kwenda kufanya kampeni kwa mwezi mzima je huwa anachukua likizo isiyo na malipo au serikali uendelea kumlipa pamoja nakwamba hayupo ofisini kutekeleza majukumu yake? Je kufanya kampeni ni moja ya excuse ambazo zinaruhusiwa kisheria kwa mfanyakazi wa serikali kuchukua likizo na je vipi kama ikitokea mfululizo wa chaguzi ndogo ndio kusema mhusika anaweza asitokee ofisini kwa mwaka mzima ili hali umma unamuitaji ? kwa kuwa kiongozi wa umma anavyofanya hivyo ushiriki ktk kuwagawa watu kwa misingi ya vyama wakati yeye ni mtumishi wa umma wote, je utumishi wake kwa umma hauwezi kuingia doa kwa kuwa ameshaonyesha bias kwa segment mojawapo ya umma? je serikali haioni haja ya mtumishi wa umma kujiuzuru utumishi wake ili haweze kushiriki kwy kampeni za siasa kikamilifu na kuwapa nafasi wanaotaka kutumikia umma kwa asilimia mia moja kufanya hivyo badala ya kumlipa mtu ambaye anashiriki ktk kuugawa umma huku akiwa amekalia ofisi ya umma ?
 
Mawaziri hawana kazi ofisini. hiki ni cheo cha kupiga bla bla tu, wenye kazi ni makatibu wakuu na ndio accounting officers.
 
Kinachokera zaidi' ni wao kutoa maneno ya kipuuzi kama haya' "mkipa wa upinzani,mim kama waziri sitoshirikiana naye kuzileta hizo Machinga complex"
 
naomba sana msaada kutoka kwa wabunge kutuulizia bungeni swali lifuatalo kuhusu mtumishi wa serikali au waziri kuacha ofisi ya wananchi na kwenda kufanya kampeni kwa mwezi mzima je huwa anachukua likizo isiyo na malipo au serikali uendelea kumlipa pamoja nakwamba hayupo ofisini kutekeleza majukumu yake? Je kufanya kampeni ni moja ya excuse ambazo zinaruhusiwa kisheria kwa mfanyakazi wa serikali kuchukua likizo na je vipi kama ikitokea mfululizo wa chaguzi ndogo ndio kusema mhusika anaweza asitokee ofisini kwa mwaka mzima ili hali umma unamuitaji ? kwa kuwa kiongozi wa umma anavyofanya hivyo ushiriki ktk kuwagawa watu kwa misingi ya vyama wakati yeye ni mtumishi wa umma wote, je utumishi wake kwa umma hauwezi kuingia doa kwa kuwa ameshaonyesha bias kwa segment mojawapo ya umma? je serikali haioni haja ya mtumishi wa umma kujiuzuru utumishi wake ili haweze kushiriki kwy kampeni za siasa kikamilifu na kuwapa nafasi wanaotaka kutumikia umma kwa asilimia mia moja kufanya hivyo badala ya kumlipa mtu ambaye anashiriki ktk kuugawa umma huku akiwa amekalia ofisi ya umma ?

majibu ya swali yatakuwa mepesi na yasiyo na mashiko, mwisho muuliza swali atazomewa na lile kundi kubwa la mrengo wa ndiyoooo!
 
Kinachokera zaidi' ni wao kutoa maneno ya kipuuzi kama haya' "mkipa wa upinzani,mim kama waziri sitoshirikiana naye kuzileta hizo Machinga complex"

ni ubinafsi wa mawaziri wa CCM na kujiona chama chao ndio chenye nchi na watu
 
Back
Top Bottom