Naomba msaada kwa huyu dada yangu maana sasa anakoelekea atatutia aibu

Kwanza; umri mzuri wa kurekebisha na kumlea vizuri binadamu yeyote yule ni kabla hajafikisha miaka 20. Akishafikisha miaka ishirini tu, inakuwa tabia yake.

Pili; anawafanyia mambo ya ajabu, kama vile kumkatisha mtoto kunyonya, kwa kuwa anajua nyie mpo, mtamjali na kumlelea wanae. Mkiendelea hivyo, msitegemee marekebisho yake yoyote.

Tatu; anawapelekesha kwasababu anajua hamuwezi kumfanya kitu chochote na anajua mnampenda. Ndio maana anafanya ujinga akijua kabisa kuwa mwisho wa siku mtampokea tu.

Kwa mtazamo wangu, suluhisho linaloweza kuwepo hapo:

Mosi; muondoeni hapo nyumbani. Kufunza mtu sio lazima tu mumng'ang'anie hapo nyumbani, muda mwingine mkimuondoa hapo atajifunza zaidi kuliko kukaa naye. Hakuna dhambi kwa kumfukuza baada ya kuwa mmejaribu kila njia ya kumsaidia na mmeshindwa.

Pili; mumwache abebe mizigo yake. Mambo ya kuwa mnamlelea watoto yanamfanya asijue majukumu yatokanayo na malezi. Muacheni ahangaike nao. Watoto wakifika umri wa kwenda Sekondari ndio mumsaidie. Hapo atajua pia kuji-control. Otherwise atakuwa anawazalia tu watoto anawaachia mlee.

Tatu; hao ndugu wako wengine waache kumuunga mkono katika mambo ya kipuuzi, kama vile kumfungulia geti. Hii tabia ikiendelea, hata wao wataanza kuona hiyo tabia ya kulala nje kama kitu cha kawaida kabisa. Mwisho wa siku na wao wataharibika.

Samaki mmoja akioza, kabla hajawaozesha na wengine, mtenge.

Ni hayo tu Mkuu.
 
Mtoa mada tafuta kazi au kama unayo tafuta mji wako hata kwa kupanga uishi Maisha yako. Wewe na huyo uliyemzungumzia wote mko sawa tu kula kulala na tegemezi katika umri mkubwa
 
Back
Top Bottom