Naomba Msaada Kufungua Kesi ya Katiba

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Waheshimiwa nimelazimika kufungua kesi ya katiba ambamo ninataka kuiomba mahakama kutoa fasiri kamili kuhusu sheria ya uchaguzi na matumizi ya Fomu namba 17.

Fomu hii kwa mujibu wa Election regulation 2010 ambayo imetamkwa katika kifungu cha 74 ina lengo la kumsaidia mpiga kura ambaye ameshindwa kutambulishwa na shahada yake kula kiapo mbele ya msimamizi wa kituo cha kupigia kura baada ya kuonywa kwamba kama maelezo yake yatakuwa ya uongo basi atakabiliwa na hukumu moja kwa moja.

Malalamiko ni kwamba kutokutumika kutokana na kutowekwa wazi lengo la kuwepo kwa fomu hiyo kumewafanya watu wenye nia mbaya kununua shahada za wapiga kura kwa lengo la kuwanyima haki ya kupiga kura. Lakini kama kwa lengo la fomu hiyo kwamba ambaye shahada yake imeharibika sana kiasi cha kushindwa kumtambulisha na yule ambaye kwa bahati mbaya amepoteza shahada yake basi ajaze fomu hiyo Na. 17 as long as jina na namba yake viko katika daftari la mpiga kura basi hatimaye atapata haki yake ya kupiga kura.

Naombeni msaada wa kisheria ili niiombe mahakama itoe tafsiri kamili juu ya matumizi ya fomu hii nikijua kwamba kwa kufanya hivyo tutakuwa ama tumefilisi au kuondoa kabisa zoezi la kununua shahada za wapiga kura.

Asanteni sana
 
Hujaelewka. Hiyo fomu no. 17 ina uhusiano gani na kununua shahada? Una maana mtu aliyeuza shahada yake anaweza kujaza hiyo fomu na akaruhusiwa kupiga kura?
 
Back
Top Bottom