mwenye shamba
JF-Expert Member
- May 31, 2015
- 972
- 1,666
Habari wana jukwaa.
Ni imani yangu mu wazima wa afya.
Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada
Mimi in kijana mwenye umri wa miaka 26, naishi Geita kijiji kinaitwa lwamgasa.
Nilikuwa nikifanya kazi kwenye migodi midogo ya dhahabu(ikumbukwe Mara nyingi tunafanya kazi kwenye mazingira hatarishi mfano vumbi, mwingiliano wa watu na urahisi wa kuambukizana magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa kama T.B).
Hivyo nilijikuta nimeambukizwa T.B,awali nilianza kukohoa taratibu, mwili ukawa unakosa nguvu na joto Kali wakati was usiku.
Hali hiyo ilidumu kwa muda wa miezi miwili na haikuathiri sana utendaji kazi wangu kwani nilikuwa nikienda kwenye dispensary napimwa na kupewa tu dawa za kuzuia kikohozi na mafua
Hali ilibadilika usiku wa tarehe 12 mwezi wa 7 mwaka ambao tumeuaga Jana kwani nilikohoa mabonge ya damu, ikabidi niende hospitali ya mkoa ndipo wakabaini nina ugonjwa wa kifua kikuu.
Nilianzishiwa dozi ya vidonge vinne kwa siku kwa muda wa miezi miwili kabla ya kubadilishiwa dozi ya miezi minne ya mwisho
Nilizuiliwa kufanya kazi ngumu, ikumbukwe kuwa maisha yangu yamejikita zaidi kwenye kazi ngumu kama kulima na uchimbaji wa madini.
Hivyo kiasi kidogo kilichokuwepo kama akiba nilimpa mke wangu aongezee kwenye biashara yake ya genge.
Kwa bahati mbaya sana mke wangu alikuwa mjamzito, pia nae nilimwambukiza hiyo T.B, ufanisi kwenye biashara ukapungua na mwisho akaacha.
Kukatisha urefu wa mada,nimejitokeza hapa kuhitaji msaada japo niweze kuhudumia familia yangu kwa huu mwezi mmoja wa matibabu uliosalia ili nisiitese familia yangu.
Nahitaji msaada wa laki moja ili ninunue chakula nikiwa nasubiri kumaliza dozi ili noendelee na kazi, akiba yangu imeniishia na mke ni mjamzito.
Kwa atakaye guswa 0755322031.
Cc @skyeclat Mshanajr Nifah GENTAMYCINE Jambazi @kassie
Sent using Jamii Forums mobile app
Mrejesho,
Nimepata msaada kutoka kwa msamalia humu humu,kanitumia sh elfu 12,bado nahitaji msaada wenu