Naomba msaada kazi yoyote ya halali

Empirically

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
238
86
Habari za saizi wakuu? Mimi ni kijana wa kiume mwenye elimu ya diploma kozi ya ualimu, lakini bado sijafanikiwa kupata kazi.Hivyo naomba kazi yoyote ya halali ambayo itaniwezesha kupata hela ya kujikimu kimaisha au kuishi mbali na nyumbani.

Mimi nipo Mvumi, wilaya ya Chamwino, Dodoma. Nipo tayari kufanya kazi mahali popote hata Dodoma hii hii lakini tofauti na ninapoishi.

Mikoa ya karibu Kama Iringa, Morogoro, Singida ambapo nauli ni nafuu kama kazi itapatikana huko nashukuru.Lakini nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote hata ya mbali Mungu akisaidia nauli ipatikane, haina shida.

Natanguliza shukrani wakuu.
 
Samahani kwa kuandika habari yote kwa aya moja sijajua namna ya kuruka mistari maana huwa siandiki habari sana
 
Back
Top Bottom