Dawa na njia mbadala za Kupunguza unene/uzito | Weight Loss techniques and advice

Samahan,ndugu zangu !kuna unene wa asili? Kwamba hata utumia njia zote haiwezekani pungua*

Mimi nilikua nawo huo wa asili, ila nimepmbana mpaka nimepungua sana, hamna dawa ya kupunguza unene tuache kudanganyana, mbinu ni moja tu, mazoezi na kupunguza wanga basi.
Mazoezi haswa ya kukimbia, sema watu wengi hukata tamaa mapema, hutegemea kupunguza unene ndani ya wiki moja, hii ni shughuli ambayo unapaswa kuwa mvumilivu, pambana, kimbia mara nne kwa wiki, ila anza kwa kutembea tembea kisha ongeza kukimbia taratibu mdogo mdogo, usianze kwa mihemko.
Ilinichukua mwaka mmoja kupunguza kilo 35kgs, nilikomaa nikafanya kukimbia kama sehemu ya maisha yangu, siku ikipita sijakimbia yaani mwili huzingua, huwa nahisi hovyoo sana.
Pia punguza msosi wa jioni, kama lazima, basi kula matango, hakikisha kuna masaa kama kumi hivi hujala kitu, yaani chakula cha mwisho kula 6pm kuanzia hapo usile kitu mpaka asubuhi.
Kumbuka kuwa mvumilivu usiyekata tamaa, kuna wakati nilikua nayafanya yote hayo mwezi unaisha nikipima nakuta nimeongeza uzito badala ya kupungua. Lakini sikukata tamaa, maana mwili huwa unajua namna ya kujilinda, kuna wakati unagoma haupungui kitu licha ya yote hayo, wakati huo huwa unafanya balance fulani za kujilinda, unatunza mafuta bila kuyatumia, ila ghafla utashangaa ipo wiki utapungua hata kilo tatu kwa mpigo.
Mwezi wote huu nimepambana sana wiki zimeenda kila nikipima nakuta nimeongeza, ila leo nimepima nikakuta nimepungua kilo moja ghafla, na wala sio kwamba nimebadilisha aina ya mazoei au msosi, yaani mwili wenyewe unakwenda utakavyo.
 
Fanya sana mazoezi..kimbia utoke jasho sana..na mazoezi ya viungo kwa sana..kunywa maji mengi mm napiga lita nne kwa siku...nakula chochote kwa kiwango chochote...kasoro soda na chips tu..pia situmii vilev....yan ww piga maziez na kunywa maji mengi..hutahitaji mambo mengi ww mwenyew utaona
 
Nenda Hospital Kwa Wajuzi Vinginevyo Ukifika Miaka 30
Utakuwa Unatembea Na Kiti Cha Kukalia Unapochoka
Muda Huu Ndiyo Ufanye Udhibiti
 
Habari zenu wakuu,

Namshukuru Mungu mwezi January nilifanikiwa kujifungua salama baby Girl. Tatizo lilonileta kwenu baada ya miezi 3 nimeongezeka uzito kupita kawaida, uliopelekea kupata maumivu ya visigino nikisimama kwa muda na magoti nikichuchuma ulaji wangu ni WA kawaida Tu milo mitatu.

Maziwa ninayo yakutosha natamani nipate mbinu au vyakula vya Kula vitakayonisaidia nisiendelee kunenepa zaidi au nipungue Ila maziw yaendelee kutoka maana hajaanza kula chochote zaid ya nyonyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom