Naomba msaada dawa ya ugonjwa wa kutoka vinyama sehemu ya haja kubwa

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Ndugu zangu wanajf, naomba msaada dawa ya ugonjwa wa kutoka vinyama sehemu ya haja kubwa na kunakuwa na maumivu makali sana muda mwingine.
 
Kitaalamu huitwa hemorrhoids (bawasiri) na zinatibika kulingana na utokeaji wake so hiyo sehemu ni sensitive sana mkuu kuna mishipa mingi hapo ukifanya makosa tu na kutegemea dawa za jf utakuja kupata kansa .
Kikubwa nenda kachekiwe hospitali kisha utapewa dawa na vitaisha vyote.
 
Pole sana mkuu.
Huo ugonjwa unaitwa BAWASIRI ni vyema ukaenda kumwona daktari japo wengi huwa wanaona aibu kutokana na sehemu yenyewe uliopo.

Matibabu yake yanategemea na hali ya ugonjwa wenyewe, kuna dawa jina la utani wanaita ROKETI kitaalam SCHERIPROCT Suppositories. Hizi dawa unaingiza sehemu ya njia ya haja kubwa kwa maelekezo ya daktari.
Aina ya pili ya matibabu ni UPASUAJI. Kwenye hii uwe makini maana Daktari wengi siku hizi njaa kali, huwa wanakimbilia upasuaji hata kama ugonjwa haujafikia kiwango hico ili wapate mshiko mzito
 
Back
Top Bottom