Naomba msaada au ushauri juu ya Fundi wa Nissan X-trail

Bonlove

Member
Feb 2, 2012
45
4
Habarini na poleni na majukumu,

Ninaomba msaada/ Ushauri juu ya Tatizo la gari langu (Nissan X- trail) nimetumia hili gari zaidi ya miaka 6, shida ilijitokeza kwenye Engine nikafanya uamuzi wa kubadilisha Engine na gear box (niliweka nyingine).

Baada ya kukamilisha hilo zoezi cha ajabu (shida) ni kuwa gari inachanganya kwenye Rejeta (Maji na gear box oil) sijajua cha kufanya fundi amejaribu kutengeneza zaidi ya mara 3, bado tatizo ni hilohilo.

Naombeni Msaada (ushauri) na kama kuna fundi mzuri wa gari aina hii (nissan x - trail) naomba namba yake.

Gari ipo Temeke (Kurasini)
 
Mie siongei mambo mengi. Nenda Kijitonyama barabara ya mabatini ukishapita kituo cha polisi, mbele kidogo mkono wa kulia kuna garage jina silikumbuki vizuri ila kuna neno Star. Hautajuta.

Walinirekebishia gari kwa bei ambayo sikuamini na hadi leo sijajutia jamaa aliyenielekeza kwao. Mie haikua X-trail lakini ni Nissani. Aliyenielekeza kwao alikua na X-trail nayenyewe walimaliza mzizi wa fitna.
 
Shukrani kiongoz
 
Back
Top Bottom