Naomba mnisamehe kama na mimi nilivyowasamehe walionikosea 2013, HERI YA MWAKA MPYA 2014

Watz tunachukulia sana Siasa na kuweka mioyoni mwetu kana kwamba siasa ndo msingi wa maendeleo yetu, au siasa ndo 100% inatufanya masikini...je, kwani msingi wa maendeleo si ni kazi? Chris Lukosi kutokana na posts zake au kukosana na viongozi wa CHADEMA au kujiondoa yeye CDM si ni maamuzi yake jamani? Je, wewe au mimi tunaichukia sana CCM lkn simchukii kila mtu atakae jitoa CDM...Watz waga hatuheshimu maamuzi ya Mtu binafsi..Swali la kichokozi..Je, Chris Lukosi kwa nini anarushiwa sana makombola hasa humu JF? kwa ajili ya maamuzi yake kujitoa CDM au nini hasa? mie binafsi siipendi siasa na kuchukiana ila siasa za hoja, ziogombane hoja sio mimi na wewe....Tusameheane by Chris Lukosi na heri ya mwaka mpya 2014...
 
Last edited by a moderator:
Heri ya mwaka mpya mbeba maboksi mwenzangu:usa2:

Lukosi box2.jpg
Mwenzio kazichanga NAULI mwaka mzima sasa yuko Kalenga anakula vitu Organic, wewe je?
 
Watz tunachukulia sana Siasa na kuweka mioyoni mwetu kana kwamba siasa ndo msingi wa maendeleo yetu, au siasa ndo 100% inatufanya masikini...je, kwani msingi wa maendeleo si ni kazi? Chris Lukosi kutokana na posts zake au kukosana na viongozi wa CHADEMA au kujiondoa yeye CDM si ni maamuzi yake jamani? Je, wewe au mimi tunaichukia sana CCM lkn simchukii kila mtu atakae jitoa CDM...Watz waga hatuheshimu maamuzi ya Mtu binafsi..Swali la kichokozi..Je, Chris Lukosi kwa nini anarushiwa sana makombola hasa humu JF? kwa ajili ya maamuzi yake kujitoa CDM au nini hasa? mie binafsi siipendi siasa na kuchukiana ila siasa za hoja, ziogombane hoja sio mimi na wewe....Tusameheane by Chris Lukosi na heri ya mwaka mpya 2014...

Ishu kubwa inayofanya huyu Mnyalu Chris Lukosi aandamwe humu ni Rambirambi za Mwangosi, alizigeuza Lambalamba. But tumeishasameheana ingawa msamaha ungeswii zaidi kama angepita kwa Mjane wa Mwangosi na kuomba msamaha. Sisi wana JF tunampenda jamaa yetu Lukosi na tumemvumilia kwenye mapungufu yake mengi, kwa minajiri hiyi tunaweza kumchangia jamaa yetu amlipe mjane wa Mwangosi na kuutua mzigo once and for all
 
Mkuu ngoja nikachukue akaunt details zangu niziweke hapa ili watu mnichangie

Pia nawashukuru kwa kunichagua kuwa mkuu wa kitengo cha rambi rambi
 
Mkuu ngoja nikachukue akaunt details zangu niziweke hapa ili watu mnichangie

Pia nawashukuru kwa kunichagua kuwa mkuu wa kitengo cha rambi rambi

Mkuu usisahau ahadi yetu ya MAGARI YA KUZOA TAKA MANISPAA YA IRINGA. Ahadi ni deni hata kama utakuwa unatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CDM chini ya kamanda Msigwa. Maadam umerudi weka sawa hii ahadi
 
Mkuu usisahau ahadi yetu ya MAGARI YA KUZOA TAKA MANISPAA YA IRINGA. Ahadi ni deni hata kama utakuwa unatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CDM chini ya kamanda Msigwa. Maadam umerudi weka sawa hii ahadi
Mkuu huu ndio mwaka ninaorudi rasmi nyumbani

Narudi Kalenga, kwa baba yangu.

Narudi Iringa kulikomboa jimbo langu

Narudi kutimiza ahadi zangu zote nilizotoa hapa jukwaaani na zile ambazo ziko moyoni mwangu

Najua siku nikionekana live pale Mjini utajua tu kuwa nimerudi

Tusubiri katiba kwanza ili msije mkaniingiza choo cha kike
 
Home office wanakutafuta Chris wewe pimbi
Hizo stori mbona za kizamani sana?

Wewe bado unawaogopa hao watu? basi uko nyuma sana

Watu wanaongelea kurudi nyumbani kuchukua jimbo wewe unawaza karatasi??? huko tulipita miaka mingi sana na sasa tunaangalia jinsi ya kuwafanya watu kama wewe wajitambue
 
Ndugu zanguni,

Sasa mwaka 2013 ndio unakatika na ni masaa machache tu kabla hatujaingia mwaka mpya 2014

Ningependa kutumia fursa hii kuwashukuru wale wote walionisapoti mwaka huu 2013 bila kusahau wagonga like na wale walioniwezesha kulitumia jukwaa hili kutoa maoni yangu.

Nawashukuru sana bodi nzima ya Jamii forums kwa kutuwezesha sisi watanzania wadogo kwa wakubwa, walio ndani na walio nje, chadema kwa ccm na wengineo kuweza kupata fursa ya kutoa maoni yao juu ya siasa za nchi yetu. Mungu awabariki na kuwaongezea busara za kuzuia machafuko na mupate uwezo wa kujua na kufuta thread yoyote itakayoleta madhara kwa jamii kwani sasa JF ni kubwa mno na ninaamini hata viongozi wetu hutembelea sana hapa.

Pia nawaomba wale wote niliowakwaza kutokana na coments zangu hapa jukwaani kwani najua kabisa kuwa coments zangu zinaweza kuwa nzuri kwa kambi yangu lakini zikawa mwiba mchungu upande wa pili. Naomba mnisamehe kwani bila kuelezana ukweli hatutafika.

Mimi pia nawasamehe wale wote hata walioniita mwizi wa rambi rambi nilizotoa mfukoni mwangu kujazia kidogo walichotoa akina chadema UK.

Baada ya hayo yote naomba niwatakie heri ya mwaka mpya 2014.

Namuomba Mwenyezi Mungu alijalie taifa letu amani kipindi hiki kijacho ambapo tutakuwa tunaingia kwenye katiba mpya

Namuomba Mwenyezi Mungu amzidishie hekima Rais wetu na bunge la katiba waweze kutuletea katiba itakayomnufaisha kila mwananchi bila kubagua Chama au dini.

Namshukuru sana Rais wetu kwa kutuletea katiba mpya

Ndugu zanguni, pia nningeomba viongozi wengine wa kisiasa waige mfano wa waheshimiwa Anna Tibaijuka, Mmwigulu Nchebma, Dr Wilbroad Slaa , Zitto Kabwe , Hamis Kigwangala na wengineo kwa kuamua kujumuika nasi kwenye jukwaa la siasa kuchangia hoja na kubadilishana mawazo kwani naamini kuwa hapa pamoja na kuwa kuna mbulumundu wengi lakini pia kumejaa great thinkers ambao mawazo yao yakisikilizwa yanaweza kusaidia katika kurekebisha pale panapopwaya nchini

MUNGU AWABARIKI WOTE

MUNGU IBARIKI TANZANIA

MUNGU TUEPUSHE NA MACHAFUKO NA UENDELEE KUTUJALIA UWEZO WA KUVUMBUA RASILIMALI ZAETU KAMA MAFUTA NK 2014

ASANTENI.

Chris Lukosi.... kalenga - Iringa

Sawa mkuu kwani mtu mwenye matatizo ya akili hajuwi akifanyacho hivyo ni muhimu kumsamehe. Nakusamehe tena kwa mara ya 77.
 
Nina shaka kama unaweza kumaintain ombi lako walau kwa 36 hrs,binafsi msamaha wangu uu nawe kiroho safi!
 
Ili JF izidi kupiga hatua zinahitajika opposite ideas za kila namna kutoka kwa 'waasi wa JF' kama lukosi, malaria sugu, FFoxy etc......
 
Pia nawaomba wale wote niliowakwaza kutokana na coments zangu hapa jukwaani kwani najua kabisa kuwa coments zangu zinaweza kuwa nzuri kwa kambi yangu lakini zikawa mwiba mchungu upande wa pili. Naomba mnisamehe kwani bila kuelezana ukweli hatutafika.

Kwa mara ya kwanza nasoma post yako nzuri mkuu, nimeipenda na zaidi ya yote kuwasamehe wengine na kuomba msamaha. Nashukuru kwa kunisamehe kwa kuwa najua kwa njia moja ama nyingine ntakua nimekukwaza.

Nichukue fursa hii pia kuwaomba msamaha wana JF wote nilowakwaza kwa comment au majibu ambayo huenda hayakuwafurahisha.

Niwatakie heri ya mwaka mpya 2014
 
Mmkuu maisha ni kusameheana, kama kungekuwa hakuna kusameheana wengi tungechinjana
 
Back
Top Bottom