Naomba mnisaidie connection ya kazi au Internship, nina Shahada ya Uhasibu

Navy seal soldier

Senior Member
Oct 6, 2019
148
272
Habarini wakubwa,

Nimekuja kwenu nikiamini kwamba JamiiForums ni sehemu inayokutanisha watu wengi tofauti tofauti, waliojikita katika nyanja na sekta tofauti, hivo nimeona ni sehemu sahihi ya kutanua network yangu na kupata msaada juu ya hili swala.

Mimi Ni kijana fresh graduate ninayeishi katika mkoa wa arusha. nimehitimu shahada ya uhasibu kutoka katika moja ya taasisi za elimu ya juu hapa nchini.

Nimekuja kwenu kuomba msaada wa connection ya kupata kazi au internships katika field ya uhasibu, fedha, ukaguzi, masoko n.k

Vile vile nna skills za kufundisha masomo ya biashara (bookkeeping, commerce, and accountancy) kwa O-level na advanced level, hivo kazi ya ualimu wa masomo ya biashara naiweza na naimudu vizuri.

Kipindi Fulani niliwahi kufanya field katika kituo kikubwa cha forodha hapa nchini ( customs), hivyo nina uelewe mpana kidogo juu ya maswala ya forodha pamoja na clearing and forwarding, nina uzoefu kidogo juu ya maswala ya clearing and forwarding, naweza kufanya kazi katika hi sekta pia.

All in all kutokana na uhalisia wa maisha ya Sasa kuliko kukaa bure naweza kufanya kazi yoyote bila kuchagua muhimu tu iwe kazi ya halali ( legal in eyes of law )

Binafsi naamini uaminifu ndio mtaji mkubwa katika Kila kitu

Makazi na makao yangu ni jijini Arusha

Kwa mawasiliano zaidi napatikana kwa 0657288997 au 0734017643

" When we all help one another every body wins "
 
Bora unisaidie wew kusema, cjui Ni wap nimeongea alichokisema funzadume
hapa ndipo uliongea sijui kuandika "Nimekuja kwenu kuomba msaada wa connection ya kupata kazi au internships katika field ya uhasibu, fedha, ukaguzi, masoko n.k". Halafu me niko upande wako nakutetea maana jamaa anataka ukafanye kazi baa wakati wewe ni mhasibu graduate
 
Je una soft skills gani zingine

Zitaje Kama computer basics , graphics design,electrical and electronics fixing .

Computer maintenance , and so on .

Utakuwa marketable zaidi
 
Mkuu peleka CV yako TAESA wako opposite na CBE Dar es Salaam, wote wanaojitolea kwenye taasisi za umma na baadhi za kampuni binafsi wanachukuliwa hapo.
 
hapa ndipo uliongea sijui kuandika "Nimekuja kwenu kuomba msaada wa connection ya kupata kazi au internships katika field ya uhasibu, fedha, ukaguzi, masoko n.k". Halafu me niko upande wako nakutetea maana jamaa anataka ukafanye kazi baa wakati wewe ni mhasibu graduate
Refer paragraph ya 6 katika hiyo thread yang
 
Back
Top Bottom